Emmanuel Mohamed - Maelezo
IMEELEZWA kuwa kubeba ujauzito katika umri mdogo, kutokuwa na uzazi wa mpango wa uzazi pamoja na magonjwa yatokanayo na uzazi ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha kupunguza vifo vya akina mama hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo, na Mke wa Rais mama Salma Kikwete, Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mpango kasi wa uwezeshaji wanawake na wasichana.
Amesema kuwa wasichana walio beba ujauzito katika umri mdogo wanaweza kupata matatizo mara mbili hadi mara tano zaidi na kusababisha vifo.
“Tutafakari kwa kina na tujiulize, je tufanye nini kuwazesha wanawake na wasichana waondokane na matatizo hayo?”
Mama Salma, amefafanua kuwa malengo ya mpango huo ni kuboresha maeneo ya elimu kwa wasichana, usawa wa kijinsia na uzazi wa mpango kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1999 na mwaka 2010 vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 147 hadi 81 kwa kila vizazi hai 1,000;
Hata hivyo vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi vimepungua kutoka 578 kwa kila vizazi hai laki mmoja hadi kufikia 454.
Tawimu hizo, zimetolewa leo na Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Mhe.Dk.Hussein A Mwinyi, wakati wa kumkaribisha mgeni rasmi Mama Salma kuzindua mpango huo;
Amesema kuwa Serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii ina mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na matatizo ya uzazi na vya watoto.
DK.Mwinyi, ameongezea kuwa mpango mkakati wa Afya ya Uzazi kwa vijana umelenga kutoa huduma ya elimu na taarifa kuhusu afya uzazi ambao unalenga kupunguza kupata ujauzito katika umri mdogo.
Wakati huohuo ,Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angelah Kariuki ametoa rai kwa wanawake kujitokeza kutoa maoni ya katiba kuhusu utungaji wa sheria ya kuzuia unyanyasaji wa kijinsia.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment