WAKAZI
wa Kibamba, Kinondoni, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, wamezikimbia
nyumba zao baada ya kutokea kishindo kikubwa cha milipuko katika Kambi ya Jeshi
la Vifaru ilyoko Mloganzila,Kisarawe, Pwani.

Tukio
hilo limetokea kati ya saa tano na 7:04 usiku ambapo milipuko hiyo ilikuwa
mitano, ikiambatana na kukatika kwa umeme, mawasiliano ya simu pia kukiwa na
mvua kubwa.

Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Fullshangweblog, wakazi hao walisema tukio hilo
limewashtua kwasababu halijawahi kutokea katika miaka zaidi ya saba walioshi
kwenye neo hilo.

Walisema
waliamua kukimbia na kuelekea kusikojulikana kwa ajili ya kuokoa maisha yao.

Mmoja
wa wakazi hao Mhando Yahaya alisema Wakazi wote wa Kibamba walikimbilia kwenye
kijiji kidogo cha Kibwegele ambapo waliamua kuacha nyumba pamoja na mali zao
bila kujali.

“Ujuwe
serikali inabidi itowe angalizo kabla na siyo kufanya siri kwa kuwa matokeo ya
siri ndiyo kama haya wananchi tunatishika na kukimbia hovyo usiku huu, mvua na
giza vikituandama ”alisema Yahaya.

Naye
Egnes Habiyu, alisema milipuko kama hiyo, imesababisha baadhi ya wagonjwa wa
moyo kushtuka hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu na kuanguka kwenye maji ya
mvua ilyokuwa ikinyesha.

Alipotakiwa
kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo, Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali, Kapambala
Mgawe alisema hayo yalikuwa mazoezi ya kawaida na hayana uhusiano wowote wa
kivita.

Vilevile
aliwatoa wasiwasi wananchi kuwa milipuko hiyo haina madhara bali ni moja ya
mazoezi ya kawaida hivyo wawewatulivu.

Kanali,
Mgawe alisema taarifa zilitolewa kwa wakazi wanaoishi jirani na kambi hiyo,
bali kwakuwa yalifanyika usiku kukiwa kumetulia kumesababisha sauti ya milipuko
hiyo kusikika mbali.

No comments:
Post a Comment