Thursday, August 23, 2012

WAZIRI: VYUO HAVIZALISHI WAHASIBU WABADHILIFU

Ukosefu wa maadili katika kazi za uhasibu na utawala vinasababishwa na muhusika kukosa uzalendo na maadili ya kazi na si chuo husika.
          Naibu waziri wa Viwanda Biashara na Masoko Mheshimiwa Gregory Teu ameyasema hay oleo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa website ya Chuo Kikuu Huria OUT pamoja na Programe tatu za masomo ya Utawala, Fedha na Biashara ambayo yatakuwa yanatolewa katika ngazi ya diploma hadi masters chuoni hapo.
          Mheshimiwa TEU amebainisha kuwa changamoto zilizopo katika fani ya uhasibu ambazo ni pamoja na kutoa matokeo mabaya katika hesabu za serikali havitokani na chuo alichosoma mhasibu bali ni watu kukosa mioyo ya kizalendo.
          Amefafanua kuwa vyuo vya elimu ya juu nchini vimeweka misingi mizuri ya masomo kwa wananvyuo ili kupata wanataaluma bora nchini.
          Aidha amesema kuhusu ushindani wa kuelekea katika soko huria vijana wa kitanzania ili wawe imara katika soko hilo wanatakiwa kuvitumia vyuo vyao vya nyumbani badala ya kuwaachia wenzao kutoka nje ya nchi katika kujiendeleza kielimu.
          Ameongeza kuwa chuo kikuu huria  hivi sasa kimejitanua ndani na nje ya nchi hususani afrika mashariki hivyo jamii ya kitanzania inatakiwa kuwa kipaumbele ili kupata misingi ya elimu ambayo serikali imeiweka.
          Pia amesema serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imeweka mikakati ya kuhakikisha inaifikisha nchi katika kipato cha kati ambayo ni pamoja na kujenga viwanda, kutafuta masomo na kufanyabiashara ili kufikia lengo iliyojiwekea.
         Chuo Kikuu Huria OUTS kipo katika maazimisho ya kusherehea za miaka 20 ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992.

Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment