Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akipokea funguo ya basi la mahabusu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde katika fupi ya kukabidhi mabasi kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Fidelis Mboya kwa niaba ya Jeshi la Magereza. Programu ya Maboresho katika Sekta ya Sheria iliyopo ndani ya Wizara ya Katiba na Sheria imetoa magari madogo matano na mabasi saba kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika leo katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (wa tatu kutoka kulia) wakikagua sehemu ya magari madogo yaliyokabidhiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusindikiza msafara wa mabasi yanayosafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (Wa kwanza kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (Wa pili kulia) wakikagua sehemu ya mabasi makubwa yaliyokabidhiwa na Wizara ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kusafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani. Kulia ni Mratibu wa Programu ya Maboresho katika Sekta ya Sheria, Emmanuel Mayeji.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (Watatu kutoka kulia waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Fanuel Mbonde (Wanne kutoka kushoto waliokaa) pamoja na Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiwa katika picha ya pamoja baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya magari ya kusafirisha mahabusu pamoja na magari madogo ya kusindikiza msafara wa mahabusu hao wakati wanapopelekwa Mahakamani na kurudishwa Gerezani. Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Gereza la Keko, jijini Dar es Salaam .
No comments:
Post a Comment