Na.Datus Boniface.
Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba (pichani) amesema uhuru wa demokrasia na haki za binadamu uliyopo duniani kwa sasa, umesababisha kutengenezwa na kutolewa kwa filamu chafu inayokashifu dini ya kiislam duniani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Sheikh Simba amesema wanaalani filamu hiyo, lakini wameitaka serikali ya Marekani itunge na kupitiw sheria ya uhuru wa maoni kwa lengo la kuzuia kejeli kama ilivyotokea katika utengenezaji wa filamu hiyo.
“Hili ni tamko la Bakwata ambalo limejadiliwa na Baraza la Ulamaa Taifa, filamu inachochea chuki, uhasama wadini mbalimbali, tumesikitishwa na kuhuzunishwa kwani lengo lake ni kumvunjia heshima Mtume”amesema
Ameenda mbali zaidi na kutaka serikali ya Marekani kupiga marufuku kurushwa kwa filamu hiyo ikiwa ni pamoja na kuongea na wamiliki wa mitandao ya kijamii waweze kuiondoa.
Hata hivyo Bakwata ilitaka kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa wale wote waliohusika kuitengeneza filamu husika.
No comments:
Post a Comment