Wednesday, September 19, 2012

RASIMU YA UDHIBITI DAWA BANDIA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YAJA



 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo,(kushoto) na  Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Raymond Wigenge. 
----
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Chakula na Dawa(TFDA,Haiiti Sillo  amesema kwamba  kamati maalum inayoaandaa  rasimu za awali   ya mifumo wa kuoanisha  usajili wa dawa  katika nchi za Afrika Mashariki(EAC)  imeshaanza kazi  hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika  kipindi cha miaka  miwili ijao.


Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi huyo  wakati akizungumza na waandishi wa habari  katika mkutano wa Ushirikiano wa wafanyabiashara wa  kutoka nchini China na Tanzania  kuhusiana na kampuni hizo uliofanyika kwenye hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini Dares Salaam.


Mkutano huo  wenye lengo la kutoa elimu kwa wanaotaka  wafanyabiashara hao kutoka nchini China wanaotaka kuwekeza katika sekta hiyo.


“Nchi za EAC zinategemee dawa nyingi kutoka nje . Rasimu hiyo itasaidia kuongeza ushirikiano wa kudhibiti  dawa bandia kwa pamoja,” .  utaratibu huu utakuwa na msharti  yanayofanana katika nchi zote ,alisema  Sillo.


Alisema mifumo hiyo itasaidia kupunguza gharama za usajili wa dawa na kuwezesha wananchi kupata dawa zilizo bora na uhakika.


 Sillo  aliwataka waombaji wa kusajili kampuni za utengenezaji dawa na vifaa tiba kuaandaa maelezo  yanayotosheleza  katika kukidhi  viwango vya  ubora na usalama wa bidhaa hizo ili kuepusha ucheweleshaji wa usajili huo.


 “ Changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni  waombaji wa usajili wa kampuni hizo kutokidhi viwango vya ubora na usalama wa bidhaa hizi. Hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwataka waombaji  wahakikishe kuwa kabla ya kuwasisilisha maombi ya usajili wahahakikishe maelezo yao yanajitosheleza,” alisema.


Alizitaja changamoto nyingine ni kuwa kutokuwepo kwa watafiti wa kutosha kutathimini ubora na usalama wa dawa , hata hivyo alisema  suala hilo wanalifanyia kazi ili kuongeza rasilimali watu ya kutosha. Changamoto nyingine ni kutokuwepo kwa ripoti za kuonyesha dawa zilizoleta matatizo kwa watumiaji  kutoka kwa watoa huduma za afya  na watengenezaji wa dawa hizo.


Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Regina Kikuli Sillo aliwataka wafanyabiashara hao kuunda mtandao utakaowasaidia kubadilishana  uzoefu katika sekta hiyo.


Naye Makamu wa Rais wa Chama cha wafanyabiashara wa  uingizaji na usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China, Meng Dongping alisema wanatengeneza bidhaa hizo  ambazo ni bora na kwa gharama nafuu ukilinganisha na nchi nyingine zilizoendelea.


 Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika  na nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo kwa upande wa  nchi za EAC.


 Makamu Rais huyo aliongeza kuwa, katika kipindi cha miezi sita  cha  mwaka 2012  ukuaji wa soko  bidhaa hizo  nchini Tanzania ,umefikia dola za Marekani  milioni 32.61 sawa na asilimia  47 .

No comments:

Post a Comment