Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
SERIKALI iko katika mikakati ya kuandaa mitaala kwa ajili ya somo la maadili, ili lianze kufundishwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu kwa lengo la kukabiliana na ukiukwaji wa maadili.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus, alipokuwa akizindua mradi wa uhamasishaji, uwajibikaji na uadilifu ulioanzishwa na Taasisi ya Save the Society.
“Tatizo la ukiukwaji wa maadili linaanzia ngazi ya familia hadi taifa, si Serikali peke yake yenye jukumu la kukuza maadili, tunahitaji wadau wengine washiriki kukabiliana na tatizo hilo.
“Serikali baada ya kuona tatizo hilo linaendelea kuwa kubwa siku hadi siku, imeandaa mikakati ambayo iko katika hatua za kati ya kuhakikisha somo la maadili linafundishwa kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu,” alisema.
Alisema mikakati hiyo inashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, ambapo kwa pamoja wanaandaa mitaala ya kufundishia somo hilo, lakini haijajulikana litaanza kufundishwa lini.
Naye Makamu Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Frank Soteri, alisema panapokosekana uadilifu na uwajibikaji, rushwa, ufisadi na ubinafsi hutawala na kukwamisha maendeleo.
“Taasisi kwa kuzingatia nafasi na umuhimu wa uongozi bora na uadilifu katika kukua kwa uchumi wa nchi, tumeamua kuanzisha kampeni hii ambayo itakuwa endelevu kadiri taasisi na taifa letu tunavyoishi.
“Tunaamini viongozi na watumishi bora wa umma, huandaliwa tangu mwanzo, kwa hiyo taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuchangia kuandaa viongozi watakaoleta mapinduzi chanya ya kiuchumi kwa nchi yetu.

Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment