Thursday, September 20, 2012

TUME YA UCHAGUZI TAIFA YAVIONYA VYAMA VYA SIASA DHIDI YA LUGHA CHAFU.



Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mh. Jaji Mstaasfu Damiani Lubuva wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini. 
Mkurugenzi Jullius Mallaba akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mdogo wa madiwani kata 29 Tanzania.
Wadau waliohudhuria kikao hicho. 
Picha Juu na Chini ni Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho.
Na Datus Boniface.
Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi  (NEMC ) Jaji mstaafu Mh . Damian Lubuva amevionya vyama vya siasa kuwa, hawatavumilia tabia ya baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kutoa lugha chafu za kashfa dhidi ya wagombea wengine au vyama kipindi cha kampeni.
Onyo hilo amelitoa jijini Dar es salaam, katika mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa.
 “tume haitavumilia tabia hiyo ambayo si ya kiistarabu, inachochea vurugu, wadau wanapoona wamedhalilishwa kwa lugha ya kashfa wapeleke malalamiko mara moja kwa kamati ya maadili katika kata husika”alisema
Awali, kaimu katibu mkuu wa chama cha U.D.P, Isaac Cheyo, alisema daftari la wapiga kura ni bovu kutokana na kuchanganya taarifa za wapiga kura kwa kata tofauti, hali iliyonyima fursa wananchi kupiga kura.
Naye, mwenyekiti wa chama cha N.l.D, Dk. Emmanuel Makaidi alibainisha utendaji mbovu wa tume ya uchaguzi akidai kwa kipindi cha mwaka jana imekuwa na kesi 47 za malalamiko juu ya chaguzi.
Alisema NEC kwa kipindi hicho imefanya madudu zaidi ambayo ilikuwa ikisimamiwa na viongozi waliopita akiwemo Rajabu Kiravu.
Hata hivyo aliongeza kuwa siyo jambo la kushangaza watendaji hao kuachia ngazi kwa pamoja kutokana na mdudu hayo waliyoyafanya.
Alienda mbali zaidi na kusema, kwa kipindi hicho NEC ilifanya madudu kwa kuchakachua uchaguzi mzima ikiwa ni pamoja kubadilisha kwa nembo za vyama vya siasa bila taarifa.
Alihoji kuwa ikiwa NEC inanyoshewa kidole na kila madau iweje uhalali wake wa kuendelea kufanyakazi nchini.

No comments:

Post a Comment