Leo Jumamosi Dec 29 ni mwaka mmoja tokea mtangazaji wa kwanza wa kike kutangaza mpira katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati Halima Mchuka (pichani) kufariki dunia.
Halima Mchuka atakumbukwa kwa weledi wake wa hali ya juu katika tasnia ya utangazaji, hasa wa mpira ambapo aliweza kubuni maneno na majina mengi ambayo yanatumika hadi hii leo, mfano mkubwa ni 'mpira umeenda fyongo' akimaanisha mpira umepigwa vibaya na mchezaji.
Leo saa kumi jioni kutakuwa na kisomo nyumbani kwa dada yake Mwajuma Mchuka Mbezi Beach, Dar es salaam. Karibuni wote kumuenzi na kumuombea dua shujaa huyu.
No comments:
Post a Comment