Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia vijana wa kitanzania nafasi za mafunzo na kazi kama ifuatavyo :
KOZI ITAKAYO FUNDISHWA : NGO MANAGEMENT & OPERATION.
SIFA ZA MWOMBAJI NAFASI :
1. Kijana wa kitanzania mwenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 45.
2. Elimu ya kuanzia kidato cha sita na kuendelea.
3. Aliye na malengo ya kufanya kazi katika taasisi zisizokuwa za kiserikali zilizopo nchini Tanzania.
4. Anayeweza kusoma na kuelewa kwa njia ya masafa marefu.
LENGO LA KOZI HII :
i. kumuandaa mhitimu kufanya kazi katika taasisi zisizo kuwa za kiserikali katika maeneo ya ubunifu, uandishi na usimamizi wa miradi yenye kuvutia na kushawishi wafadhili
( Designing, Developing & Managing Donor Funded Projects )
ii. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa katika taasisi zisizokuwa za kiserikali katika maeneo ya utafutaji na utengenezaji wa fedha za kukuza mfuko wa taasisi husika.
( Designing, Managing & Developing Fund Raising Programmes )
iii. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi kwa ufasaha mkubwa katika taasisi zisizokuwa za kiserikali kama mtafiti wa tafiti za aina mbalimbali kama vile tafiti za kijamii, tafiti za mazingira, tafiti za kisheria nakadhalika.
iv. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi katika taasisi zisizokuwa za kiserikali kama msimamizi na mratibu wa miradi na shughuli mbalimbali za taasisi husika.
v. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi katika taasisi zisizo kuwa za kiserikali kama mwalimu wa somo la ujasirimali, uongozi wa biashara pamoja na utengenezaji wa bidhaa za aina mbalimbali kwa njia ya nadharia kama vile sabuni, chaki, mishumaa, batiki nakadhalika.
vi. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi kama msimamizi wa shughuli za katika taasisi zisizokuwa za kiserikali zinazojihusisha na masuala ya uwekaji na ukopaji wa pesa ( VICOBA & SACCOSS ) pamoja na usimamizi wa uundwaji wa taasisi za aina hiyo.
vii. Kumuandaa mwanafunzi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali kama mtoa elimu ya ukimwi, mazingira na uraia. n.k.
MUDA WA MAFUNZO : Mafunzo haya yatafanyika kwa muda wa miezi mitatu. Mwezi mmoja utakuwa ni mafunzo kwa njia ya nadharia na miezi miwili itakuwa ni mafunzo kwa njia ya vitendo ambayo yatafanyika katika taasisi zisizo kuwa za kiserikali.
BAADA YA KUHITIMU : Wahitimu wa mafunzo haya, watapata nafasi ya kufanya " internship " kwa muda wa miezi sita, katika miradi mbalimbali inayo ratibiwa na taasisi mbali mbali zisizokuwa za kiserikali nchini Tanzania kwa kutumia ujuzi walioupata katika mafunzo haya.
ADA YA MAFUNZO : Ada ya mafunzo haya ni nafuu sana.
Tuma maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo-kazi haya kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.comm.
Maombi yaelekezwe kwenda kwa :
Mkurugenzi Mtendaji,
RafikiElimu Foundation,
Centre For Distance Learning Programme.
S.L.P 35967,
Dar Es salaam.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 08 JANUARY 2013.
Mafunzo yataanza, tarehe 14 JANUARY 2013.
Tunapokea maombi kutoka waombaji waliopo katika wilaya zote za Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment