Friday, May 9, 2014

PLUIJM ABWAGA MANYANGA MANYANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Kocha, Hans Van Pluijm (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo jana kuhusu kuiacha Yanga na  na kwenda Saudi Arabia kuifundisha klabu ya Al Shoala. Katikati ni Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu na mwisho ni ofisa habari wa timu hiyo, Baraka Kizunguto.

Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amebwaga manyanga kuendelea kuinoa timu hiyo baada ya kupata ‘ofa’ ya kuinoa klabu ya Al Shoala Sports ya Saudi Arabia.
Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga jana, Pluijm alisema ofa hiyo ni kubwa na roho inamuuma kuicha Yanga ambayo tayari ni mwanachama, lakini hana jinsi.
“Ofa ni kubwa sana, yeyote asingevumilia na nimezungumza na viongozi wa Yanga, wamekubaliana na hilo.
“Naondoka kwenda Ghana mchana huu kuwasaidia Yanga kusaka wachezaji ambao watawasaidia msimu ujao. Nitahakikisha nawatafutia wachezaji wazuri kuliko hawa walionao.”
Pluijm ameinoa Yanga kwa miezi sita na kuiwezesha kushika nafasi ya pili, na alisema tayari ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja na Al Shoala Sports.
Akifafanua kuondoka kwake iwapo ametofauatina na viongozi, Pluijm alisema: “Nina masikitiko moyoni kuiacha nchi nzuri ya Tanzania. Ninawashukuru wote, wachezaji, wanachama, viongozi wa Yanga na Watanzania wote kwa ujumla. “Kabla sijaja kuifundisha Yanga, meneja wangu alipata ofa kubwa Saudi Arabia na nikasaini mkataba wa mwaka mmoja, lakini uongozi wa timu ninayoenda kuifundisha (Al Shoala), walikuwa na matatizo na kocha aliyekuwapo, hivyo wakaniomba nisubiri mkataba wake uishe ndiyo na mimi nijiunge nao.
“Mkataba wake umeisha na mimi naanza kazi rasmi Julai. Mkataba wangu utamalizika baada ya mwaka mmoja. Itategemea kama Yanga watakuwa bado wananihitaji, na kama ofa yao itakuwa nzuri, nitarudi.”
Naye katibu mkuu wa Yanga, Benno Njovu alisema wamebariki kundoka kwa Pluijm kwa vile tayari alishapata kazi Saudi Arabia na ameshasaini mkataba, hivyo wapo kwenye harakati za kusaka kocha mwingine wa kuziba pengo la kocha huyo, ambaye alianza kazi Januari akichukua mikoba ya Ernie Brandts.
Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment