Wednesday, July 9, 2014

MASHINE HUDUMA MACHO ZAFUNGWA HOSPITALI SHREE HINDU MANDAL

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Dk. Kaushik Ramaiya
 
Watanzania sasa hawatotumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi kutafuta huduma za macho, baada ya Hospitali ya Shree Hindu Mandal ya jijini Dar es Salaam kufunga mashine nane za kisasa za kutoa huduma hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital hiyo, Dk. Kaushik Ramaiya, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, kufungua kitengo cha kutolea huduma hiyo.

Alisema kuanzishwa kwa kituo hicho kutasaidia kupunguza gharama za kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hiyo.

“Ugonjwa wa kisukari, presha vimekuwa vikiwasababishia watu wengi kupata upofu wa macho kutokana na kukosa uwezo wa kupata matibabu ya haraka kwenda nchi za nje.

Lakini kuanzishwa kwa huduma hizo hapa, Watanzania wengi watanufaika sambamba na kufanyiwa upasuaji na kukwanguliwa macho kama watakuwa hawaoni vizuri,” alisema.

Alisema ugonjwa wa macho umekuwa ukiwasumbua watu wengi na wengine kupoteza uwezo wa kuona na kuwa vipofu, lakini kutokana na kupatiwa mashine hizo zenye thamani ya dola za Marekani 400,000 zilizotolewa na Dk. Kanubha Babla kutoka Mombasa, Kenya, kutawasaidia kupata matibabu yaliyobora na salama.

Kaushik alisema jengo hilo litakuwa mbali na kutoa huduma za macho, pia litakuwa linatoa huduma za kisukari, figo na kutumia ‘lenzi’ na kutoa miwani kwa wale wenye matatizo.

Naye Dk. Rashid aliipongeza hospitali hiyo kwa kupata mashine zenye viwango vya juu vya kutoa huduma hiyo.
Alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa huo husababisha upofu kwa asilimia 20.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment