Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Agnes Mtawa akisalimiana na Prince Akishino wakati alipowasili Hospitalini hapo. Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Dkt. Mahadhi Juma Maalim.
Prince Akishino na Mkewe Princess Kiko wakifurahia jambo katika mojawapo ya wodi za watoto ambazo zimekidhi viwango vya program ya uboreshaji wa huduma.
Mkuu wa Idara ya Afya ya Akina Mama Dkt. Mathew Kallanga akitoa ufafanuzi kwa Prince Akishino kuhusu idara yake inavyowahudumia akina mama.
Princess Kiko akifurahia na akina mama baada ya kuona mtoto aliyekuja kliniki.
*****
*****
Mwana
wa Mfalme wa Japan Prince Akishino na mkewe Princess Kiko leo
wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuona jinsi inavyotoa
huduma zake kwa Watanzania.
Akitoa
salamu za pongezi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili Bi. Agnes Mtawa amesema Hospitali imekuwa na uhusiano wa muda
mrefu na Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo la JICA katika maeneo
mbalimbali ya huduma ikiwemo ujenzi wa maabara maalumu ya watoto, ujenzi
wa Kituo cha Maelezo ya Afya Muhimbili pamoja na kuongeza uwezo wa
Hospitali katika kuboresha huduma zake kupitia mpango wa uboreshaji
huduma (quality improvement program).
Katika
ziara yao, wametembelea Jengo la watoto kitengo cha watoto walioungua
moto, wodi ambazo zimekidhi viwango vya ubora wa huduma, na jengo la
wazazi ili kuona namna ambavyo akina mama wanapata huduma za afya ya
mama na mtoto.
No comments:
Post a Comment