Tuesday, May 19, 2015

BIL 4/- KUBORESHA BARABARA DAR

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

SHILINGI bilioni nne zinatarajiwa kuanza kutumika kurekebisha maeneo korofi yaliyoharibiwa na mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema hayo jana alipokuwa akijibu hoja za wabunge katika makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya Sh trilioni tano, ambayo yalipitishwa na Bunge.
Pinda alisema tayari Mkoa wa Dar es Salaam umeshawasilisha maombi ya Sh bilioni tisa kwa ajili ya kuripea miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko, na yeye ameshaagiza Hazina ianze kutoa kama Sh bilioni nne za kuanzia.
Mbali na kutoa fedha hizo, Pinda alisema amezungumza na Rais Jakaya Kikwete juzi ambaye ameliagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kushiriki katika kazi hiyo hasa katika kujenga madaraja.
Wakati akijadili makadirio ya bajeti hiyo, Mbunge wa Viti Maalumu, Zarina Madabida (CCM), aliitaka Serikali itenge fedha kwa ajili ya marekebisho ya barabara zilizoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Chanzo:Habari Leo

No comments:

Post a Comment