
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano

Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana Jealous Chirove, akielezea mafanikio ya mradi

Naibu
waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti
cha kutambua mchango wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa
ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira
kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.
.jpg)
Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma,
Zanzibar.ndugu Ameir Ali Ameir akizungumza na waandishi wa habari.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na waandishi wa habari.

Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.

Baadhi
ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa
Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO).
ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia
ujasiriamali. Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka
5 toka kuanzishwa kwa mfuko wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa
kongamano katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.
Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika
kutengeneza ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi
pamoja na kuongeza ushindani kwenye uchumi wa Afrika.
Mradi ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza
ujasiriamali na kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu,
kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji wa mtaji. Kwa kupitia mradi huu wa
Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulilenga
kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za Kenya, Tanzania na
Uganda.
Msingi mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni
mwa vijana, kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza
uwingi wa mambo yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha
taasisi za vijana kutekeleza mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha
upatikanaji wa mitaji kwa vijana walio nje ya shule.
Toka mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni
wajasiamarali wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara,
kusaidia uanzishwaji wa biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji
wa zaidi ya ajira 40,000 kwa vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka
malengo ya mradi yaliyoaninishwa mwanzo.
Pamoja na hayo, mradi pia umewezesha:
· Zaidi ya biashara 16,000 zimeanzishwa ikiwa ni matokeo ya elimu ya biashara
· Zaidi ya kazi 30,000 zimetengenezwa
· Zaidi ya vijana1,000,000 wamefikiwa kupitia vyombo vya habari (radio, magazeti) na majukwaa mengineyo.
· Zaidi ya wajasiariamali 30 wa mfano wametangazwa
· Zaidi ya wanafunzi 50,000 wamepata elimu ya ujasiriamali
· Zaidi ya walimu 340 wa shule za msingi, sekondari pamoja na vyuo wameendelezwa
· Jumla ya tathmini 6 zimefanyika pamoja makongamano 3 ya kisera
· Miradi 33 imefanyika na taasisi za vijana
· Zaidi ya vijana 30,000 wamepata elimu ya biashara
Akizungumza wakati wa kongamano, Mshauri Mkuu wa Ufundi wa Mradi, Bwana
Jealous Chirove alisema tathmini yao kwenye mradi imeonyesha kuwa zaidi
ya asilimia 50% ya vijana waliopata elimu ya biashara wameweza kuanzisha
biashara ndani ya miezi 12 huku wastani kila biashara ikitengeneza
ajira mbili.
‘Mradi umepata mafanikio makubwa kwani kwa Tanzania pekee zaidi ya
biashara 10,000 zimetengenezwa ambazo zimepelekea zaidi ya nafasi za
ajira 20,000 ambazo kwa hakika ni mchango mkubwa katika kupambana na
tatizo la ajira hapa nchini’ alisema Chirove.
Mafanikio mengine ya mradi ni uanzishwaji wa mradi wa Kazi Nje Nje ambao
unawatumia wahitimu kutoka vyuoni kuwafikia vijana walio mtaani na
ujumbe kuhusu ujasiriamali pamoja na uanzishwaji wa mashindano ya
kuandika mradi wa biashara uliowafikia moja kwa moja zaidi ya vijana
70,000.
Mgeni rasmi wa Kongamano hili ambalo limehudhuriwa na wadau mbalimbali
ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga
amepongeza mchango wa ILO na Mfuko wa Ujasiriamali kwa mradi wao huu.
‘Tatizo la ajira kwa vijana bado ni changamoto kubwa kwa nchi
zinazoendelea na bara zima la Afrika kiujumla hasa kutokana na ongezeko
kubwa la wahitimu kutoka katika vyuo mbaliumbali hapa nchini, hivyo
tunaishukuru ILO na serikali ya Denmark kwa juhudi zao za kuisaidia
serikali kumaliza tatizo hili’ alisema Mheshimiwa Mahanga.
Mheshimiwa Mahanga alisema mpaka sasa ni asilimia 25 tu ya watu
wanaoingia kwenye soko la ajira ndio wanaajiriwa kwa mwaka kwenye sekta
binafsi.
No comments:
Post a Comment