Basili Mramba,Daniel Yona,Agrey Mgonja mwingine hakufahamika jina lake
wakijadili jambo kabla ya kusomewa hukumu yao ambayo imeahirishwa mpaka
tarehe 6 mwezi wa 7.
Daniel Yona, Agrey Mgonja wakisubiria hatima ya kesi yao inayowakabili katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar.
Ndugu na jamaa waliofika mahakamani hapo kusikiliza hukumu hiyo.
Mramba na wenzake wakijadili kabla ya hukumu yao ambayo imeahirishwa tena
Kesi ya matumizi mabaya ya fedha za serikali ya awamu ya tatu chini ya
Rais Benjamini Mkapa inayowakabili viongozi waliokuwa kwenye dhamana
katika sekta mbalimbali akiwemo Waziri wa Fedha Basil Mramba,Waziri wa
Nishati na Madini Daniel Yona, na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Agrey
Mgonja imesogezwa mbele baada ya mwenyekiti wa jopo la Majaji John
Utamwa kushindwa kufika Mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo kwa
dhurula ya ugonjwa kwa ruksa ya daktari kwa siku mbili.
Akitoa taarifa hiyo mbele ya mahakama, Hakimu Mkazi, Mheshimiwa Sauli
Kilemela amesema kuwa kutokana na sababu za kiafya zinazomkabili
mwenyekiti hawana budi ya kuahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 6 mwezi huu
majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutoa hukumu.
Kesi hiyo inayowakabili akina Mramba inasemwa ni kwa sababu ya
kulisamehe kulipa kodi Kampuni la Alex Stewart na kuisababishia serikali
kupoteza kiasi cha shilingi bilioni 11.7
Na GPL
No comments:
Post a Comment