Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Frank
Mvungi
Shirikisho
la vyuo vya elimu ya juu Tanzania linaloundwa na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi limesema kuwa miongoni wa wanachama 42 walioomba kuteuliwa kugombea
urais kupitia chama hicho hakuna aliye maarufu au mwenye nguvu kuliko chama
hicho.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Bi. Zainabu
Abdalah Issa wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
“Shirikisho
la vyuo vya elimu ya juu tuna imani kubwa na wajumbe wote wa vikao vyote vya
maamuzi ndani ya chama chetu kwa kuwa watatuteulia mgombea safi, muadilifu, na
mzalendo atakayedumisha umoja na mshikamano ndani na nje ya chama
chetu”alisisitiza Zainabu.
Akifafanua
bi Zainabu amesema watia nia 42 wana Nafasi sawa katika uteuzi ambapo ni jambo
la wazi kuwa wapo watakaokidhi vigezo na wapo watakaoshindwa kwa kuzingatia
kanuni na taratibu za uteuzi ndani ya chama cha mapinduzi (CCM).
Pia
Zainabu alitoa wito watia nia wote 42 kuwa mgombea atakayepitishwa na vikao
vyote vya maamuzi ndio atakuwa mgombea wetu wote na itakuwa ni jukumu la kila
mwanachama kumsemea na kumnadi kwa Watanzania wenzetu ili CCM iendelee kuongoza
Tanzania.
Akizungumzia
mfumo wa kutoa maamuzi ndani ya chama cha mapinduzi Zainab amesema kuwa CCM ni
Taasisi iliyoundwa kwa Muundo wa kuongoza kwa pamoja na kutoa maamuzi kwa
pamoja dhana inyodhihirisha kuwa Chama cha mapinduzi si mali ya mtu binafsi au
taasisi ya mtu mmoja inayotarajiwa kumfurahisha mtu huyo.
Shirikisho hilo linakipongeza chama hicho, kwa
kuendelea kutekeleza demokrasia kwa vitendo kwa kuwapa wanachama wake kushiriki
kwenye nafasi zote za uongozi ndani ya chama kwa ajii ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi
octoba 2015.
No comments:
Post a Comment