Mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi wa
kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi
Julius Mamilo (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul
Makonda, ripoti ya ukaguzi huo Dar es Salaam leo asubuhi. Ukaguzi huo
ulifanyika katika kipindi cha miezi miwili kwa kuwahusisha wataalamu wa
masuala ya ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (kushoto), akizungumza na wanahabari baada ya kupokea ripoti hiyo.
Mwenyekiti wa kamati
ya ukaguzi wa kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya
Kinondoni, Mhandisi Julius Mamilo (ushoto), akitoa ripoti hiyo kwa
wanahabari mbele ya DC Makonda.
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda, amempa siku 14 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni kumpelekea taarifa kuhusu ujenzi wa barabara mpya ambazo
zimeharibika kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Makonda ametoa maagizo hayo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipokea taarifa ya
ukaguzi wa kiufundi wa barabara za lami katika Manispaa ya Kinondoni
iliyotolewa mbele yake na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi, Mhandisi
Julius Mamilo.
Makonda alisema kwa muda wa miezi miwili aliunda kamati iliyofanya uchunguzi wa kuharibika kwa barabara hizo na kubaini makosa.
Makonda alisema sababu ya kuharibika kwa
barabara hizo ni kutokana michoro yake kutokuwa sahihi na sheria ya
wazabuni kutofuatwa, huku usimamizi wa mikataba haioneshi kama miradi
ilisimamiwa ipaswavyo.
"Hata suala la kuthamini uwezo wa
wataalamu wa wakandarasi halikuwepo, pia mkataba wa kazi waliofanya na
malipo waliopata, hakuna nyaraka ya kuthibitisha hayo," alisema.
Alisema katika kufanikisha mchakato wa
uchunguzi wa barabara zilizoharibika, waligundua barabara ya Polisi
Mabatini, Akachube ziliharibika kwa kiasi kikubwa, huku zikiwa na muda
mfupi tangu zitengenezwe.
"Utengenezaji wa barabara hizo
ulibainika kutumia kipindi kifupi mfano ya Akachube na Journalism
zilizojengwa kwa siku 120, ikiwa muda huo ni mdogo, kwani ilitakiwa
angalau watumie siku 365," alisema.
Alisema ubora wa unene kwa barabara ya
Polisi Mabatini haukukidhi viwango, huku kokoto zilizotumika ni ndogo
kulingana na zile zinazohitajika na kusababisha kuwa nyembamba tofauti
na ilivyotakiwa.
No comments:
Post a Comment