Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wauguzi wakiwa katika wodi iliyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia
wagonjwa wenye dalili za kipindupindu katika Hospitali ya Mwananyamala,
Dar es Salaam, jana. Picha na Salim Shao.
Dar es Salaam. Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu ulioikumba Dar es Salaam, imeongezeka na kufikia watatu.
Mgonjwa wa tatu alipoteza maisha jana huku wengine wawili wakifariki
dunia juzi. Hadi sasa wagonjwa 34 wamelazwa wakisubiri vipimo
kujiridhisha kama wana ugonjwa huo.
Wagonjwa wanne waliokuwa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mwananyama vipimo
vyao vimeonyesha kuwa wana ugonjwa huo na wamehamishiwa kwenye kambi
maalumu iliyoko katika hospitali hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda alisema jana: “Tunachofanya ni kutoa elimu kwa wananchi kupitia
mabwana na mabibi afya, ili kuhakikisha wagonjwa hawaongezeki,
ikiwezekana kuzuia kabisa maambukizi mapya kwa namna yoyote ile.”
Makonda alisema ofisi yake inaboresha kambi iliyopo kwenye Kituo cha
Sinza Palestina ili kuwaweka wagonjwa watakaogundulika kuwa na ugonjwa
huo kutoka maeneo jirani na hapo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Aziz Msuya, alisema kambi maalumu
kwa ajili ya wagonjwa hao ya Mburahati ipo tayari na wameshahamishia
ikiwa tayari na wagonjwa 11 kutoka Mwananyamala.
No comments:
Post a Comment