Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) anayewakilisha
vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
Amri hiyo ilitolewa jana na Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova,
katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, baada ya Lowassa kuanza ziara
yake juzi ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam
kushuhudia kero zinazowakabili wananchi.
Kova alisema marufuku hiyo inatokana na jeshi hilo kugundua kuwa
kuna wagombea ambao wameanzisha mtindo wa kutembelea maeneo mbalimbali
jijini hilo yakiwamo vituo vya daladala, masoko na mengine kwa madai ya
kuyatembelea makundi ya watu wenye kipato cha hali ya chini.
Alisema polisi imebainika mikusanyiko mikubwa isiyotegemewa inaashiria uvunjifu wa amani.
“Wakati wa ziara za aina hiyo yamejitokeza makundi ya watu
mbalimbali kama vile waendesha bodaboda, machinga na makundi mengine
katika namna ambayo imeleta taharuki pamoja na usumbufu unaotokana na
kelele, msongamano au shughuli za usafiri kusimama kabisa,” alisema
Kova.
Alisema juzi mchana katika makutano ya mtaa wa Swahili na Uhuru,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Lucas Mkondya, alikutana na
Lowassa ili kumpa hadhali ya kiusalama.
Kova alisema Mkondya alishindwa kutekeleza jukumu hilo kwa sababu
Lowassa alikuwa amezungukwa na waendesha pikipiki wasiopungua 40 na
magari mengi na kusababisha msongamano katika eneo hilo.
“Msongamano huo ulileta athari na malalamiko kutoka kwa watumiaji wengine wa barabara jijini Dar es Salaam,” alisema.
Kova alisema jeshi hilo lilibaini kuwa Lowassa alianza kuzunguka
katika maeneo ya Wilaya ya Temeke kuanzia Agosti 24, mwaka huu kwa
kutumia vyombo vya usafiri zikiwamo daladala.
“Ni lazima ieleweke wazi moja ya kazi za Polisi ni kudhibiti
makundi makubwa ya watu katika namna ambayo kiongozi yeyote wa aina ya
wagombea urais anatakiwa kulindwa kipindi chote cha kampeni hadi siku ya
uchaguzi,” alisema.
Alisema ni vema wagombea hususani wa urais wakaonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea.
Vilevile, Kova aliwataka wagombea hao kujihadhiri kwenda katika makundi yasiyo rasmi kwa sababu za kiusalama.
“Tunawashauri viongozi wa vyama na wagombea wao wafuate ratiba za
kampeni za mgombea urais/mgombea mwenza kwa vyama vya siasa kama
ilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuondoa hisia za kufanyika
kampeni nje ya ratiba,” aliongeza.
LOWASSA AKATISHA ZIARA
Wakati huo huo, Lowassa jana aliendelea na ziara yake ya kukagua kero zinazowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Ziara hiyo ilifanyika zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya Ukawa
unaoundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, CUF na NLD, kuzindua
kampeni za mgombea wao wa urais jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo iliyoanza saa 3 asubuhi, Lowassa alitembelea
masoko ya Tandale, Tandika na Kariakoo ambayo hata hivyo, haikuimaliza
kutokana na kuzongwa na umati.
Lowassa ambaye jana kama ilivyokuwa juzi aliambatana na mgombea
mwenza, Juma Duni Haji na baadhi ya maofisa wa Chadema, walilazimika
kukatisha ziara hiyo kimya kimya, baada ya Kamanda Mkondya kuzuia
msafara wake kwa sababu zilizodaiwa kuwa ni za kiusalama.
Akiwa katika mtaa wa Swahili Kariakoo, saa 6:15 mchana, msafara huo
ulizuiliwa na Polisi ambao walikuwa wakiwasiliana na baadaye Kamanda
Mkondya alilazimika kumfuata Lowassa kwenye gari lake na kuzungumza
naye.
Lowassa alifuatwa na Kamanda Mkondya, kwenye gari hilo Toyota Noah
yenye namba za usajili T 607 DDR, na kumueleza kuwa msafara huo haukuwa
salama kutokana na kuzongwa na umati huo.
Kamanda Mkondya, ambaye alitumia takribani dakika 5 kumuelewesha
Lowassa, alisema hakuwa na taarifa ya ziara hiyo na kwamba watu wengi
walikuwa wameanza kumfuata, hivyo kumshauri aahirishe kwa ajili ya
usalama wake.
Aidha, aliagiza msafara wa magari kugawanyika ili kupisha shughuli kuendelea kufanyika sokoni hapo.
Magari hayo yalianza kutawanyika kutoka mtaa huo kisha gari
alilipanda Lowassa kungia mtaa wa Kongo ambako lilizidi kufuatwa na
umati uliokuwa ukiimba ‘Lowassa rais’.
Kufuati agizo hilo, gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari,
lilifuata barabara ya kuelekea Mnazi Mmoja na kuongozana na magari
mengine yaliyokuwa kwenye msafara wa kiongozi huyo.
ATEKA MASOKO
Lowassa na Duni waliwasili katika soko la Tandale saa 3:20 asubuhi na kupokelewa na umati ambao haukuwa na taarifa ya ujio wake.
Umati huo ulikuwa ukiimba ‘Rais rais’, ‘unasubiri kuapishwa tu’
‘hakuna haja ya kupiga kura’ waliendelea kufanya hivyo na kulisukuma
gari lake Tandale sokoni hadi stedi ya daladala Argentina.
ANYWA MAZIWA YA MAMALISHE
Akiwa sokoni hapo, Lowassa alikabidhiwa kikombe cha maziwa na mama
lishe wakati akipita njia hali iliyomlazimu kuyachukua na kunywa.
Baada ya kupokea maziwa hayo na kuanza kuyanywa, wananchi walianza
kushangilia huku wakiendelea kuimba na kutembelea wauza nafaka, mama
lishe na wafanyabiashara ya matunda.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Tandale, Mutabu Ally, alimueleza Lowassa kuwa
wanakutana na changomoto mbalimbali zikiwamo za kupanda kwa bei ya
bidhaa na kukosa faida huku miundombinu ya soko hilo ikiwa mibovu.
Aidha, Ally hakusita kuelezea hisia zake kwa Lowassa kwa wanamuunga
mkono na kumuakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
Oktoba, mwaka huu.
TANDIKA WAFUNGA BIASHARA
Baada ya kuwasilia katika soko la Tandika wilayani Temeke,
wafanyabiashara na wateja wake walikumbwa na taharuki na kuacha shughuli
zao kwenye kumlaki Lowassa.
Lowassa ambaye aliwasili sokoni hapo majira ya saa 4:30 asubuhi,
alisababisha wafanyabiashara na wateja wao kulazimika kukimbia kwenda
kumuona.
Nao wafanyabiashara wa maduka walilazimika kufunga maduka yao kudhibiti vibaka kupora bidhaa zao na fedha.
ASHINDWA KUKAGUA BIASHARA TANDIKA.
Katika soko la Tandika, Lowassa alishindwa kufanya ukaguzi kama alivyofanya soko la Tandale kutokana na kufunikwa na umati.
Lowassa alitumia dakika 30 kutembea sokoni humo huku wananchi
wakitangulia mbele yake wakiendelea kuimba nyimbo za kumuunga mkono.
Walisikika wakiimba ‘mkombozi wa watanzania’, ‘mziki wa lowassa
kuutuliza haiwezekani’ waliendelea kufanya hivyo na katika mitaa
aliyopita ya Malumba wananchi walionekana wakitoka ndani na kuunga
msafara huo wa waliokuwa wakimshangilia.
Pia, katika msafara huo wafuasi wake walibeba ndoo kichwani wakimaanisha wanashida ya maji.
Wengine walichukua magauni aina ya ‘Dela’ yaliyovalishwa sanamu ambalo lina nembo za CUF na kuanza kumsindikiza nalo.
BODA BODA WAAMSHA HISIA
Katika maeneo ambayo Lowassa alipita katika barabara za Tandale,
Morogoro, Mburahati, Kigogo, Tabata, Mandela, Tandika, Kurasini Shimo la
Udongo, madereva bodaboda waliomuona walianza kumfuata huku
wakishangilia.
Mbali na kuzuiliwa na walinzi wakihisi wanaweza kusababisha msafara huo kuzuiliwa, walizidi kumfuata.
WALINZI WAZIDIWA NGUVU
Katika mitaa ya Tandika sokoni, Lowassa na Duni walifuatwa na umati
na kusababisha walinzi wake kuzidiwa na nguvu ya watu waliokuwa
wakikimbia na kusababisha vumbi na kutumbukia kwenye matope.
ANUNUA MAJI YA KIROBA
Lowassa akiwa katika soko la Tandika, aliwaungisha vijana waliokuwa
wakifanya biashara kwa kununua maharage kilo 20 ambazo hata hivyo,
alishindwa kuondoka nazo kutokana na mfuko aliobebea kuchanika.
Maharage hayo yalimwagika chini na watu walianza kuyazoa, pia
alinunua maji ya viroba mawili kwa Sh. 10,000 ambayo yalichukuliwa na
vijana hao na kuanza kuyanywa na mengine kuyamwaga chini ili kumpunguzia
vumbi.
WAHAMASISHANA WATUNZE VITAMBULISHO
Katika maeneo ambako Lowassa alikuwa akishangiliwa, wananchi walikuwa wakiulizana kama wa nakadi za kupigia kura.
Walikuwa wakielezana na kuhamasishana kuwa wavitunze nyumbani hadi siku ya kupiga kura ili waiondoe CCM madarakani.
Ziara ya Lowassa ya jana inafuatia ya juzi aliyofanya ya kukagua kero za usafiri wa daladala wanazopata wananchi.
Akiwa ameambatana na mgombea mweza Duni, Lowassa alipita katika maeneo ya Gongo la Mboto, Chanika na Mbagala.
KAULI YA CHADEMA
Kufuatia kauli ya Polisi kuzuia ziara za Lowassa, Chadema ilisema
itaendelea kufanya kampeni zake kwa kufuata kanuni na sheria za uchaguzi
na kwamba nchi haiongozwi kwa maelekezo ya mtu mmoja, bali sheria za
nchi.
Mkuu wa Kitengo cha Hbari na Mawasiliano Chadema, Tumaini Makene,
alisema Polisi waeleze Lowassa amevunja sheria gani ya nchi kwa kupita
maeneo wanayoishi watu.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment