Thursday, March 10, 2016

Jukumu la kuwawezesha wanawake ni la jamii nzima – Irine KiwiaKiwia

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mkurugenzi wa kampuni ya Frontline Porter Novelli ambaye nia ni mtetezi wa haki za wanawake nchini Bi Irine Kiwia amesema katika kuhakikisha wanawake wanapiga hatua za kimaendeleo nchini ni jukumu la wadau wa maendeleo nchini kuweka mikakati endelevu kwa kushirikiana na serikali ili kuhakikisha usawa wa wanawake unapatikana.

Bi Kiwia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kuhusu siku ya wanawake dunuiani na nafasi ya wanawake katika jamii yetu.

''Wapo wanawake ambao ni wasomi na wanauwezo wa kushika nyazifa mbalimbali katika jamii ni vyema wapewe nafasi hizo siyo kwa kigezo cha mwanamke bali kutokana na uwezo wao na ujuzi katika ngazi husika''-Amesema Bi Kiwia

Vilevile Kiwia ameitaka serikali kutizama sheria ambazo bado hazitoi fursa jkwa wanawake katika kujikwamua kiuchumi na kiutamaduni mfano sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo ambayo inatoa ruhusa kwa mwanamke kuolewa akiwa na umri chini ya miaka 18.

Aidha amewataka wanaharakati na serikali kwa ujumla kuunganisha nguvu zao pamoja ili kuhakikisha haki ya mwanamke inapatikana kwa kupinga mila potofu za kumkandamiza mwanamke ambazo zimeota mizizi katika jamii.


No comments:

Post a Comment