Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ugonjwa
wa Kipindupindu umeendelea kusambaa nchini licha ya serikali kwa
kushirikiana na mashirika mbalimbali kuonyesha nia ya kupambana na
ugonjwa huo ambao mpaka sasa umesababisha zaidi ya watu 290 wamepoteza
maisha.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya
Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Neema Rusibamayila
alisema serikali imekuwa ikiendelea kutoa fedha ili kupambana na ugonjwa
huo ambao unaonekana kuzidi kuwa tishio kwa maisha ya watanzania.
Alisema
serikali imeshatoa milioni 900 kwa ajili ya kusaidia mapambano ya
Kipindupindu ambapo fedha hizo zimekuwa zikitumika kununua dawa,
kusaidia vituo vya afya ambavyo vinawahudumia wagonjwa wa Kipindupindu
na kuziwezesha timu za uelimishaji kuhusu kipindupindu kufikia maeneo
mengi zadi.
“Serikali
imekuwa ikiunga mkono mapambano na kuhusu gharama Wizara ya Afya
ilishapokea Milioni 900 kutoka hazina kwa ajili ya kusaidia kupambana na
Kipindupindu,” alisema Dkt. Rusibamaliya.
Alisema
pamoja na fedha hizo lakini pia kuna mashirikia yamekuwa yakiwasaidia
ambayo ni pamoja na UNICEF ambao wameshatumia Bilioni mbili ambazo
zilitumika kununua vifaa zikiwepo dawa za kuulia vijidudu kwenye maji,
vitanda na vituo vya kutolea dawa.
Mashirika
mengine ni CBC wao walitoa wataalamu wa afya, Red Cross walitoa vifaa,
vitanda, wataalamu wa afya na watu waliojitolea kusaidia uelimishaji na
CMF ambao nao walitoa vifaa tiba na dawa kwa wagonjwa.
Nae
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Michael John alisema katika
kipindi cha wiki moja iliyopita walipokea taarifa za kuwepo kwa wagonjwa
wapya 758 ambao ni asilimia 40 zaidi ya taarifa ya wiki mbili
zilizopita ambapo walipokea taarifa za wagonjwa 544.
Aidha
John aliwataka viongozi wa dini kutumia nafasi yao katika jamii kwa
kuwaelimisha waumini wao kuhusu ugonjwa wa Kipindupindu na waache imani
potofu kutokana na baadhi ya maeneo kuacha kuchemsha maji kutokana na
kuwa na imani ambazo siyo za kweli.
No comments:
Post a Comment