Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme ya Norway Mhe. Tone
Skogen akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa mapango wa ukusanyaji kodi
nchini kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Ashatu Kijaji.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
10/03/2016
DAR Es Salaam
Serikali
ya Kifalme ya Norway imetoa kiasi cha Dolla za kimarekani shilingi
Milion 5 kwa Serikali ya Tanzania kwa kuwaunga mkono Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) na Serikali ya awamu ya tano katika jitihada zake katika
kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.
Makubaliano
hayo ya ufunguzi wa kuchangia mapato yamefanyika leo jijini Dar es
salaam kati ya Naibu Waziri wa mambo ya Nje kutoka Serikali ya Kifalme
ya Norway Mhe. Tone Skogen pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na
Mipango Dkt Ashatu Kijaji.
Akizungumza
katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Serikali ya
Kifalme ya Norway Mhe. Tone Skogen amesema kuwa lengo la mpango huo ni
kuimarisha na kuongeza kodi ya mapato ya ndani kwa kuhakikisha kwamba mianya ya wakwepaji kodi inazuiwa.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt Ashatu
Kijaji amesema kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuwaelimisha
wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa ili
kuondokana bajeti tegemezi kutoka nje.
“Lengo la kuimarisha uelewa wa wananchi kuhusu umuhimu wa ulipaji kodi bila kushurutishwa na kuzuia mianya yote ya ukwepaji kulipa kodi ni kuondokana na utegemezi wa bajeti na kuanza kujitegemea hivyo hatuwezi kufika huko bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini” alisisitiza Naibu Waziri huyo.
Naye
Kaimu Kamishna Mkuu TRA Bw. Alphayo Kidata ameishukuru Serikali ya
Kifalme ya Norway kwa kuimarisha uwezo wa wataalamu nchini kwa
kuwawezesha mbinu mbalimbali za kukagua mahesabu katika makampuni makubwa nchini.
Awali
Serikali ya Kifalme ya Norway ilitoa zaidi ya Dola za kimarekani
million 3 katika mpango huo wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato nchini.
No comments:
Post a Comment