Mkurugenzi
wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto)
akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya
Wachezaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein 'Machinga', wakati wa
mkutano na waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika
Jumamosi hii Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi
wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji
Mkuu wa Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa
Tamasha hilo, Bahari Camari.
Mkurugenzi
wa Fedha wa Property International Hashim Thabiti (wa pili kushoto)
akimkabidhi Jezi zitakazotumika katika Tamasha hilo Naohodha wa timu ya
Wachezaji wa zamani wa Simba, Moses Mkandawile, wakati wa mkutano na
waandishi wa habari kuhusu Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii
Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Balozi wa Algeria
nchini Tanzania, Saad Balabed (kushoto) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa
Property International, George Obada na (kulia) ni Mratibu wa Tamasha
hilo, Bahari Camari.
Balozi
wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed (kulia) amkimkabidhi Tisheti
Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, zitakazotumika kufanyia
mazoezi siku ya Tamasha. (wa pili kushoto) Katikati ni Afisa Habari wa
Property, Saleh na Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International,
George Obada.
Balozi
wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed, akizungumza na waandishi wa
habari na baadhi ya wachezaji wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba,
kuhusu Tamasha la jumamosi katika Uwanja wa Uhuru.
Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
KAMPUNI ya Property International Ltd imedhamini bonanza la
uzinduzi wa kitabu cha soka cha Safari ya Soka la Tanzania litakalofanyika
Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika bonanza hilo la uzinduzi wa kitabu hicho litaambatana
na maadhimisho ya sherehe za miaka 54 ya uhuru wa Algeria, ambalo litahudhuriwa na Waziri wa
Habari Michezo na Utamaduni, Nape Nauye ambaye ataongozana na Waziri wa Mambo
ya Ndani Mwigulu Nchemba.
Katika Bonanza hilo pia kutakuwa na mechi kadhaa ikiwemo maveterani wa
timu za Simba na Yanga, mechi za vyombo vya habari pamoja na mabalozi wa nchi
mbalimbali nchini Tanzania wataungana na kucheza na maveterani wa Simba na
Yanga. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari katika
ofisi za Property zilizopo mtaa wa Shauri Moyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo ya mipango miji Masoud Khalfan, alisema wamefurahishwa kushirikishwa
katika mambo ya michezo na wako tayari kushiriki zaidi kwenye michezo.
“Kama
tungepata mapema taarifa hizi za kudhamini, tungeweza kufanya makubwa
zaidi katika bonanza hili, ila tumeamua kufanya tukio hilo kwa kiasi
kidogo ili
kutoa mchango wetu kwenye tukio hili kubwa na la kipekee kwenye historia
ya
soka la Tanzania la kuwaenzi wachezaji wa zamani, iwapo tutashirikishwa
mapema katika mengine yajayo basi tunaamini tutweza kufanya zaidi ya
haya” alisema Khalifan.
Naye balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed
alizungumza katika mkutano huo, akisema wamefurahi kusherehekea miaka 54 ya
uhuru wa nchi yao katika tukio hilo kubwa la kimichezo nchini.
“Ilkuwa tusherehekee
miaka ya uhuru wa nchi tangu Julai 15, lakini tulipopta taarifa ya tukio la
uzinduzi wa kitabu hicho na bonanza tuliamua kusogeza mbele hadi Jumamosi hii,”
alisema Balabed.
Baadhi ya wachezaji mbalimbali wa zamani wa klabu za Simba
na Yanga kama Kenneth Mkapa (Yanga), Mohamed Mwameja (Simba), Iddi Sulemani
(Simba), Mohamed Hussein ‘Mmachiga’ (Yana na Simba) Tomas Kipese (Simba), Moses
Mkandawile (Simba) walikuwemo kwenye mkutano na kila mmoja kutamba kumfunga
mwenzake.
Katika bonanza hilo maveterani wa Simba watachezana na wale
wa Yanga, kisha kutakuwa na mechi zingine kama E FM vs Bakheresa, Chanel Ten na
Wasanii wa vichekesho, Orex na Umoja wa watuma salamu, kisha mechi ya mwisho ni
maveterani hao wa Simba na Yanga kucheza na mabalozi hao.
Kitabu hicho cha Safari ya Soka la Tanzania kitakachozinduliwa
kwenye bonanza hilo, kinahusu maisha na historia ya soka la Tanzania kuanzia
mwaka 19926 hadi mwaka huu.
Mratibu Bahari Camari akizungumza.
Mchezaji wa zamani wa Simba Moses Mkandawile, akizunguma.
Beki wa zamani wa Yanga, Keneth Mkapa, akizungumza.
Kipa wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, akizungumza.
Afisa
Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada (kulia)
akizungumza na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Saad Balabed,
kumfahamisha shughuli za kampuni hiyo, wakati alipofika Ofisini kwake
leo mchana.
Afisa
Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obada akimuonesha
Balozi huyo, baadhi ya Tuzo walizopata katika maonesho ya Biashara ya
Kimataifa ya mwaka huu, Sabasaba.
Mazungumzo....
Picha ya pamoja....
Balozi
wa Algeria nchini Tanzania, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji
wa zamani wa Vilabu vya Yanga na Simba,mara baada ya mkutano huo.
No comments:
Post a Comment