|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa studio
ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa wakurugenzi wa Wanene
Entertainment Bw. Darish Pandit wakati akiwasili katika hafla ya uzinduzi wa
studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili
katika hafla ya uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29,
2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wakurugenzi
wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit (kulia) wakati wa hafla uzinduzi wa
studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam
katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo .
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akizungumza jambo na wakurugenzi wa Wanene Entertainment
Bw. Bhadresh Pandit (kushoto) na Bw. Darish Pandit(wa pili kushoto) wakati wa
hafla uzinduzi wa studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016
Jijini Dar es Salaam wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya
Wanene Entertainment Bw. Hanscana.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akikata utepe kuzindua studio
mpya ya kisasa ya Wanene Entertainment
Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam wa
pili kushoto ni mmoja ya wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish
Pandit. |
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja ya
wakurugenzi wa Wanene Entertainment Studio Bw. Darish Pandit(kushoto) kwa
kuhusu maeneo mbalimbali ndani ya studio hiyo
Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia)
akiangalia moja ya vyumba vya kurekodia na kutengengeneza video vilivyopo ndani
ya studio ya Wanene Entertainment mara baada ya kuizindua studio hiyo Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam kulia ni
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(aliyekaa) akiangalia moja ya ya kazi zilizorekodiwa na kutengenezwa na kampuni ya Wanene Entertainment Studio wakati
alipokuwa akizundua studio hiyo iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam Julai 29, 2016. |
|
Mtayarishaji wa video kutoka kampuni ya Wanene Entertainment
Studio Bw. Hanscana akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura
(aliyekaa) naamna kazi za video zinavyotengenezwa mara baada ya
kurekodiwa katika maeneo mbalimbali alipotembelea studio hiyo mara baada ya kuizindua
rasmi Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura akimpongeza mmoja
wa wakurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Bhadresh Pandit mara baada ya kutembelea
na kuzindua studio hiyo ya kisasa Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi
Joyce Fissoo akizungumza wakati wa hafla uzinduzi wa studio za kisasa za Wanene
Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam. |
|
Mkurugenzi wa Wanene Entertainment Bw. Darish
Pandit akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa studio yake
uliofanya na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia
Wambura Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Baadhi ya wadau waliohudhulia hafla ya uzinduzi wa
studio ya kisasa ya Wanene Entertainment Julai 29, 2016 Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Anastazia Wambura ( wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
wakurugenzi wa studio za kisasa za Wanene Entertainment na wa tatu kushoto ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi Joyce Fissoo na kulia ni Afisa
Utamaduni kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Musa Nyoni.
|
Picha/Habari na Raymond Mushumbusi
Wasanii
nchini wameaswa kuzingatia maaadili katika utengenezaji wa kazi zao ili kuenzi
na kulinda mila, desturi na tamaduni za
mtanzania.
Wito
huo umetolewa jana na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura wakati akizindua studio ya kisasa ya kurekodi kazi za sanaa ya
Wenene Entertainment.
Mhe
Anastazia Wambura amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa hawafati maadili
katika utengenezaji wa kazi zao na kuvifanya vyombo vinavyosimamia kazi za
sanaa nchini kama Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutoa adhabu dhidi yao
kutokana na ukiukwaji wa maadili katika kazi zao.
“Ninaiomba
kampuni ya Wanene Entertainment kuisaidia Serikali kuwaelimisha wasanii
watakaoleta kazi zao kutengenezwa kwenu kuzingatia maadili badala ya
kutengeneza kazi ambazo haziendani na maadili ya nchi yetu” alisema Mhe
Anastazia.
Kwa
upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo
amehaidi kushirikiana na studio ya Wanene Entertainment kuendeleza sanaa ya
Tanzania kufikia katika viwango vya kimataifa na kuongeza pato la wasanii na
taifa kwa ujumla.
Naye
Mkurugenzi wa kampuni ya Wanene Entertainment Bw.Darsh Pandit amesema kuwa ufunguzi wa studio hiyo
ni muitikio wao kwa Serikali ya awamu ya tano katika suala la kutoa ajira kwa vijana na kuwezesha vijana
kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao kupitia kazi za sanaa.
“Studio
hii ina lengo la kukuza na kuendeleza sanaa ambayo imekuwa ajira kubwa kwa
vijana wengi na tunaahidi kuzingatia maadili katika utengenezaji wa kazi zetu
na pia tutazingatia ubora ili kuitangaza sanaa ya Tanzania kimataifa” alisema
Bw. Pandit.
Aidha
mtayarishaji wa video katika kampuni hiyo Bw. Hasacna amesema kuwa ni fursa
sasa kwa watayarishaji wa video wanaochipukia nchini kuonesha vipaji vyao kwa
kuwa wabunifu katika uandaaji na utengenezaji wa video za muziki na filamu kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment