Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Dianna Melrose alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini.
Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimpongeza Balozi Melrose kwa kuiwakilisha nchini yake vema na kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Uingereza. Kwa upande wa Balozi Melrose, alisema anaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa anaupata kipindi chote cha uwakilishi wake. |
No comments:
Post a Comment