Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza kwa mara nyingine tena kwenye kliniki ya Bwana. Juma Mwaka (Dk. Mwaka) ili kufanya ukaguzi wa kinachoendelea katika kliniki hiyo ambayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuwa kampuni. (Kaama inavyoonekana pichani).
Dk Kigwangalla ambaye amefanya ziara ya kushtukiza katika kliniki hiyo kama alivyowahi kufanya mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo ambapo katika tukio la awali, ilielezwa kuwa Dk. Mwaka alikimbia na kumuachia Ofisi Naibu Waziri na baadae aliweza kuibuka tena na kuendelea naa shuguli zake hizo.
Hivi karibuni Julai 11 mwaka huu, mamlaka husika ziliweza kutangaza kumfungia Dk. Mwaka juu ya kuendelea na shughuli zake hizo ikiwemo kumfutia kibali chake ambapo baada ya siku mbili alirudia tena kufanya shughuli zake huku akibadilisha jina kutoka Kliniki na kuwa kampuni.
Tukiolilianza saa sita kasoro robo, ya mchana ambapo Dk Kigwangalla alifika eneo la Dk. Mwaka huku akikuta geti likiandwa limefungwa (Closed), licha ya ndani kuwa na watu wakiendelea na shughuli za tiba.
Ndani, ya kituo hicho kulikutwa na wafanyakazi watatu akiwemo Mwanaume mmoja na wanawake wawili ambao baada ya kuulizwa wahusika wakuu, wafaanyakazi hao walikana kuwapo mahala hapo ndipo Polisi walipotumia mamlaka ya kisheria ya kuamuru kufanya ukaguzi pamoja na Mamlakahusika wakiwemo TFDA, Baraza la Famasia Nchini na lile la Baraza la Tiba Asili na Tiba mbadala pamoja na Dk. Kigwangalla.
Baada ya uchunguzi wa kina ndani ya kituo hicho, walikuta madawa mbalimbali yakiwemo ya yanayotumika mahospitali huku mengine yakiwa yamesha kwisha muda wake. Mbali na dawa hizo, pia walikuta nyaraka mbalimbali za watu waliokuwa wanafika kwenye kituo hicho kupata tiba licha ya kufungiwa.
Aidha, Dk. Kigwangalla na timu yake hiyo walifanikiwa kukuta shehena kubwa ya madawa ya mitishamba ambayo imehifadhiwa kwenye chumba maalum hata hivyo, Dk. Kigwangalla alitaka dawa hizo ishikiliwe.
"Dk. Mwaka', naagiza akamatwe mara moja, ndani ya masaa 24, na afikishwe mahakamani kwa kukaidi agizo halali la Serikali la kusitisha huduma zake za tiba asili na tiba mbadala, impersonation kwa kujifanya yeye ni Daktari Bingwa wa Tiba ya kisasa wa Magonjwa ya Wanawake.
Hii ni pamoja na kukutwa na shehena ya dawa za tiba ya kisasa za aina ya 'ferrovit ' bila kuwa na vibali vya serikali, na pia kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala bila kuwa na kibali, baada ya kibali chake cha utabibu kufutwa na Serikali Julai 11, 2016” alieleza Dk. Kigwangalla.
Dk. Kigwangalla ametoa maagizo ya moja kwa moja kwa Mrakibu wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi Ilala, ambaye alikuwa kwenye zoezi hilo, Kamanda, E. M Swebe ambaye hata hivyo aliahidi kushughulikia suala hilo.
Kwa upande wake mkaguzi wa TFDA, Dk. Itikija Mwanga amesema kuwa, madawa yaliyokutwa yataendelea kushikiliwa hii ni pamoja na kufanyiwa utafiti kama ni kweli yanafaa kwa matumizi ya kibinadamu ama la pamoja na taratibu zingine.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mkaguzi wa TFDA, Dk. Itikija Mwanga wakiwa nje ya geti la kituo cha Tabibu Juma Mwaka, Ilala Bungoni, Jijini Dar es Salaam.
Jengo la Klinini ya tabibu Juma Mwaka linavyoonekana kwa nje
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiingia kwenye kliniki ya tabibu Juma Mwaka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na mmoja wa watumishi wa kliniki ya Tabibu Juma Mwaka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkaguzi wa TFDA, Dk. Itikija Mwanga na Kamanda wa Polisi, E.M. Swebe wakati wa kufaanya ukaguzi ndani ya kliniki ya Tabibu Juma Mwaka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkaguzi wa TFDA, Dk. Itikija Mwanga
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya orodha ya watu wanaopatiwa kliniki kwenye kituo hicho
Maafisa wa Polisi na TFDA wakikagua madawa yaliyokutwa ndani ya kituo hicho
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakiangalia makadi ya wagonjwa ya kliniki yaliyokutwa nchini humo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akichungulia moja ya milango iliyofungwa huku wafanyakazi wakikataa kuifungua
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwasikiliza baadhi ya wagonjwa waliofika kupatiwa dawa wakiwa ndani ya kituo hicho
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya maeneo ya kliniki hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakichungulia ndani kwenye dawa zilizokutwa zinaendelea kutumika
Baadhi ya madawa yakiwa ndani ya chumba maalum ndani ya kliniki hiyo ya tabibu ya Juma Mwaka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiendelea kukagua ndani ya kliniki ya Tabibu Juma Mwaka.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akichungulia moja ya jengo ndani ya kliniki hiyo ya Tabibu Juma Mwaka
Moja ya madawa yaliyokutwa ndani ya Kliniki ya Tabibu Juma Mwaka
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa matamko juu ya kuhakikisha Tabibu Juma Mwaka anajisalimisha mikononi mwa jeshi hilo la Polisi pamoja ndani ya masaa 24.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha wanaimalisha ulinzi ndani ya kituo hicho pamoja na kumkamata Tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka taratibu halali za Serikali.
Mkaguzi wa Chakula kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Dk Itikija Mwanga akizungumza na vyombo vya Habari juu ya tukio hilo pamoja na madawa waliyoyakuta ndani ya kliniki hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo juu ya kujisalimisha kwa Tabibu Juma Mwaka ndani ya masaa 24 kabla ya kuchukuliwa hatua kali kutokana na kukiuka taratibu za Nchi ikiwemo kuendesha huduma za kitabibu licha ya kufungiwa. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
No comments:
Post a Comment