Ikiwa
ni Takribani miezi michache kupita tangia mabasi ya mwendo kasi yaanze
kufanya kazi kwa ufanisi mzuri, kumekuwa na mambo kadha wa kadha
yakiendelea ikiwa ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu ya vituo hivyo
vya mabasi hayo.
Hili
limeonekana bila chenga Morogoro Road ambapo kipande cha kutokea
Jangwani mpaka Manzese kikionesha wazi vifaa vya kuhifadhia taka
vimeharibika, huku vingine vikionekana kuchomolewa, kupinda, na
kulegea.
Swali
la kujiuliza hapa ni kwamba kwa jinsi miundombinu hii ilivyo kaa ni
ngumu sana hata mtu kugonga kwa mguu sasa inakuwaje inaharibika kiasi
hiki?
Hapa
upande wa kulia ukionekana kuwa kifaa cha kuhifadhia taka kilisha
chomolewa na kubakiza mfuniko tuu na papo hivi kwa zaidi ya mwezi sasa.
Hapa Kifaa cha kuhifadhia taka taka kikiwa kimepinda haijulikani kiligongwa au kuna watu walikuwa wanataka chomoa.
Hiki kikiwa kimelegea kabisa amambapo muda wowote litachomoka
Hapa mfuniko ndio ulisha potea tena
Hili nalo tayari linaelekea kudondoshwa chini
Hii hapa ndio funga kazi kabisa yani wamesha chomoa muundo mbinu wote wa kushoto
Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa
No comments:
Post a Comment