Siku
za hivi karibuni kumekuwepo na tuhuma za kuwepo kwa baadhi ya Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) yanayojihusisha na kuhamasisha vitendo vya
ushoga nchini. Tunapenda kuujulisha umma kuwa NGOs zinasajiliwa
kutekeleza majukumu yanayokubalika kisheria na kwamba vitendo vya
kuhamasisha ushoga si majukumu halali yanayopaswa kutekelezwa na NGOs.
Tunazitaka NGOs kutekeleza majukumu yaliyo ndani ya usajili wao na
kuepuka vitendo vya uvunjifu wa sheria. Aidha, tunazidi kusisitiza kuwa
vitendo vya ushoga havikubaliki nchini kwani ni kinyume na mila, desturi
na sheria za nchi. Ofisi ya Msajili inaomba wadau na umma kwa ujumla
kutoa taarifa zitakazowezesha kuthibitisha tuhuma tajwa ili hatua
stahiki dhidi ya NGOs husika zichukuliwe. Taarifa zinaweza kutolewa
kupitia namba zifuatazo: 022 2110714/0222123143/ 0754391942/0715391942.
M.S.Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
01 Agosti, 2016
No comments:
Post a Comment