Meneja Mkuu wa TV1, Joseph Say akitoa utangulizi wa programu hiyo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani)
Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu akitoa ufafanuzi wa programu hiyo.
Mkuu wa Uzalishaji Vipindi wa TV1, Mukhsin Mambo akielezea jinsi kipindi hicho kitakavyorushwa.
Meneja Masoko wa Startimes, Damien Li akielezea ushirikiano wao na TV1 katika kuhakikisha Ligi hiyo inaoneshwa laivu na bure.
Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah akizungumzia uwepo wake katika uchambuzi wa Ligi Kuu ya Uingereza itakayorushwa na live na TV1
Mwendeshaji wa vipindi vya Ligi Kuu ya Uingereza kutoka TV1, Ally Kashushu akiwaahidi makubwa watazamaji na mashabiki wa soka.
Blogger
Mkongwe hapa Nchini anaye endesha Libeneke la Kajunason Cathbert Kajuna
akiuliza swali wakati wa Mkutano huo wa TV1 na waandishi wa habari
Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika Mkutano huo
Hapa waandishi wa habari wakiwa katika studio zitakazotumika kwa ajili ya kurekodia uchambuzi wa Ligi hiyo.
Mkuu wa Uzalishaji Vipindi, Mukhsin Mambo akiwaelezea jambo waandishi wa habari waliofanya ziara ya studio hizo.
Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah akiwa katika eneo ambalo watakuwa wakifanyia uchambuzi wa Ligi hiyo
Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah(Kulia) akiwa na Mwendeshaji wa vipindi vya Ligi Kuu ya Uingereza kutoka TV1, Ally Kashushu sehemu watakayokuwa wakifanyia uchambuzi huo
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
Na Chande Abdallah Dar es salaam yetu Blog
Kituo cha
Televisheni nchini, TV1 leo hii kimezindua kampeni yake inayokwenda kwa jina la
Toroka Uje ambayo inawaletea watazamaji wake matangazo ya bure ya mechi zote za
Ligi Kuu ya Uingereza maarufu kama English Premier League zitakazoanza kutimua
vumbi kuanzia Agosti 13 mwaka huu.
Akizungumzia
kampeni hiyo Meneja Mkuu wa TV1, Joseph
Sayi alisema kuwa Watanzania kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitumia pesa nyingi
kuangalia ligi hiyo maarufu duniani lakini kupitia TV1 ambayo inapatikana
kwenye king’amuzi cha Startimes, Watanzania watakuwa wakitazama mechi hizo bure
bila gharama yoyote.
Naye Meneja Masoko
wa TV1, Gillian Rugumamu aliongeza kuwa mbali na watazamaji wa TV1 kufurahia
mechi hizo ambazo zitarushwa kuanzia mechi ya kwanza hadi ya mwisho wa ligi,
pia wamejiandaa kukutana na watazamaji wa TV1 kupitia michezo mbalimbali,
matamasha na mashindano yatakayokuwa na zawadi mbalimbali zikiwemo vifurushi
vya king’amuzi cha Startimes na nyingine kibao.
Akizungumzia
kuhusu kampeni hiyo ya Toroka Uje, Mkuu wa Uzalishaji vipindi wa TV1, Mukhsin
Mambo, alisema kuwa kipindi hicho kitakachoanza
kuruka tarehe 10 mwezi huu kitakuwa katika siku tatu ambapo kutakuwa na
mijadala ya kandanda, mpira laivu na uchambuzi kuhusu mechi zijazo ambapo
uchambuzi huo utaongozwa na wachambuzi wakubwa akiwemo Dr Leaky Abdallah na
Ally Kashushu.
Aidha Meneja
Masoko wa Startimes, Damien Li aliwahakikisha Watanzania kuwa Startimes
haitaongeza bei ya vifurushi wala kutoza chochote kwa watazamaji wa Ligi hiyo
kupitia TV1 kwa kuwa ni bure kabisa.
Imeandaliwa na Blogs za Mikoa Tanzania kupitia www.blogszamikoa.com , blogzamikoa@live.com 0653146563
Ahsanteni sana na mungu awasimamie huo mpango ufanikiwe na uwe wa kudumu
ReplyDeleteSidhani kama Wataonesha mechi zote ni baadhi tu
ReplyDeleteDah hii itakuwa poa sana hongera tv 1 kwa mapinduzi makubwa,tupo pamoja sana
ReplyDeleteHongera sana tv 1
ReplyDeletemmh mbona kama siamini masikio yangu, ila kama ni kweli mungu awape wepesi katika program hiyo nzuri.
ReplyDeleteif is this true..then to hell dstv!
ReplyDelete