Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura( katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa michezo
na wadhamini wa timu ya Olimpiki ya Tanzania
mara baada ya kuiaga timu hiyo inayoenda kushiriki mashindano ya
Olimpiki nchini Brazil leo Agosti 1, 2016.
Habari/Picha na Raymond Mushumbusi
Wanamichezo
nchini wameaswa kutojihusisha na matumizi ya dawa au mbinu za kuongeza nguvu
katika michezo ili kuepuka na madhara yanayojitokeza ikiwemo kuzorotesha sekta
ya michezo.
Wito
huo umetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipokuwa akiwaaga wanamichezo wanaoenda kushiriki mashindano
ya Olimpiki kwa mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Mhe.
Anastazia Wambura amesema kuwa wanamichezo wengi duniani kwasasa wanakabiliwa
na changamoto kubwa ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu mwilini
katika michezo mbalimbali.
“Niwatake
wachezaji,madaktari na viongozi wa michezo mbalimbali kuhakikisha kuwa hakuna
mchezaji anajejihusisha na vitendo vya aibu na kwa pamoja tuungane na kupinga
jambo hili kwa kujali afya na ushindani uliopoa” alisema Mhe. Anastazia.
Aidha
amewataka viongozi wote wa michezo, waalimu na madaktari wa michezo kuungana
kwa pamoja kupiga vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni kwa kutoa
elimu kwa wanamichezo wao na wasisite kutoa adhabu kali pale inapothibitika
mwanamichezo amejihusisha na matumizi ya dawa hizo.
Kwa
upande wake katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi ameahidi
kutekeleza suala hilo kwa kutoa elimu kwa waalimu na wanamchezo juu ya madhara
ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwili katika michezo.
|
No comments:
Post a Comment