Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa
pongezi kwa Bohari ya dawa Tanzania (MSD), baada ya kufanikisha ununuzi
wa dawa kwa pamoja na moja kwa moja bila kutumia 'middle men'.
Pongezi hizo amezitoa leo jijini Dar es salaam wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya dawa, ambayo yatakuwa yanasambaza madawa na vifaa tiba nchini na kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa hivyo katika hospitali zote nchini.
''Nawapongeza
sana MSD nyinyi mnatekeleza uzalendo vizuri, nasema kwa dhati mmeanza
vizuri, mimi ni mgumu kupongeza kwahiyo kama nawapongeza mjue ukweli
mnafanya kazi, nakumbuka Mkurugenzi wa MSD na Waziri wa Afya waliniomba
fedha ili wawe wananunua dawa wenyewe bila 'Middle men' na wamefanikisha
hilo'', amesema.
Aidha
Rais Magufuli ametoa ruhusa kwa MSD kufungua maduka yao ya dawa sehemu
mbalimbali nchini, lakini wasiyakabidhi kwa halmashauri bali wayasimamie
wenyewe hata kama wataongeza wafanyakazi ni sawa tu.
Kwa
upande mwingine Rais Magufuli amewalilia wafanyabiashara nchini
kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuokoa kiasi cha zaidi ya
bilioni 500 ambazo zinatumika kununua dawa nje ya nchi kila mwaka.
No comments:
Post a Comment