Katibu
wa Itikadi, uenezi na mafunzo ya vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Taifa, Comrade Mhe. Amos Gabriel Makalla ameitaka Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuimarisha huduma ya majisafi
kwa wakazi wa Sinza wilayani Ubungo.
Ameyasema
hayo wakati mwendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam
alipofanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya TP Sinza ambapo
amesisitiza uimarishaji wa huduma ya majisafi na salama kwasababu ni
haki ya Mwananchi.
"Nawaagiza
DAWASA mjitahidi kuweza kufanikisha utoaji wa huduma ya maji kwa
wananchi hasa wa kata ya Sinza, hiyo ni haki yao kupata huduma ya maji
na tusisubiri viongozi tufike na kutatua changamoto hiyo." ameeleza Mhe.
Makalla
Hata
hivyo ameipongeza Mamlaka kwa jitihada zinazoendelea kufanyika katika
kwa utekelezaji wa mradi wa maji Sinza D ambao upo hatua ya mwishoni ya
utekelezaji wake.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hassan Bomboko ameipongeza DAWASA kwa
kuendelea kuboresha huduma ya maji kwa wananchi na kusisitiza wananchi
kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo utekelezaji wa miradi ya maji
inaenda kukamilika.
"Niwapongeze
DAWASA kwa kazi kubwa mnayoifanya ya kuendelea kutatua changamoto ya
wananchi kuhusu huduma ya maji ambayo ndio kero kubwa," ameeleza Mhe.
Bomboko.
Nae
Meneja wa DAWASA Magomeni, Julieth John ameahidi kutekeleza maagizo
yaliyotolewa na Viongozi yanayolenga kuboresha huduma ya Majisafi katika
Kata ya Sinza na maeneo mengine.
No comments:
Post a Comment