UZALISHAJI
wa nguruwe Tanzania umekuwa ukiongezeka kutokana na uboreshwaji wa
miradi unaofanywa na wafugaji nchini ambao wamekuwa wakiboresha ili
kuendana na soko lililopo kwasasa ambsalo limeonekana kukua.
Ameyasema
hayo Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Mifuko, Wizara ya Mifugo na
uvuvi, Dk. Stanford Ndibalema wakati wa uzinduzi wa mbegu mpya za
nguruwe pamoja na uhimilishaji wa nguruwe kwa njia ya mrija uliofanyika
Julai 27,2024 Jijini Dar es Salaam.
Amesema uzinduzi wa mbegu hiyo mpya utasaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa nguruwe nchini na kuweza kukuza soko.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Naberera CTK, Bi Bensolight Msaki
amesema kuwa tatizo la mbegu bora za nguruwe Tanzania litapungua sana
kutokana na uzalishaji wa mbegu hizi mpya na bora.
Aidha
amesema mbegu hizo mpya zinatarajiwa kuinua hali ya maisha ya
watanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kukua haraka pamoja na kuzaa
vibwagala (watoto) wengi na wenye afya.
Nae
Mwakilishi kutoka Bodi ya Nyama Bw. Kassimu Mnangwa amewataka wafugaji
wa nguruwe nchini kufuata taratibu za ufugaji ikiwa ni pamoja na kupata
usajili kutoka Bodi ya Nyama, ambapo usajili unafanyika kupitia mfumo
wa kielectroniki wa mimis.mifugo.go.tz.
Mbegu
mpya za nguruwe zilizozinduliwa ni majike aina ya CG36 na madume aina
ya P81 (Pietrain), P26 (Duroc) na P90 kutoka Kampuni ya Choice/Axiom
Genetics, Ufaransa.
No comments:
Post a Comment