Home » » Benki ya CRDB yatoa takwimu ya utekelezaji wa mipango ya benki hiyo kwa kipindi cha mwaka 2011

Benki ya CRDB yatoa takwimu ya utekelezaji wa mipango ya benki hiyo kwa kipindi cha mwaka 2011



Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya kifedha ya benki hiyo kwa kipindi cha mwaka 2011 na utekelezaji wa mipango yake. Kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Operesheni na Huduma kwa Wateja, Philip Alfred na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma Shirikishi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya maofisa wa benki hiyo.

MKURUGENZI Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei amesema hatua ya serikali na wanasiasa kuingilia kati na kuwaamulia wakulima juu ya masoko ya mazao yao, kunasababisha wakulima hao kukosa faida.

Aidha, kitendo hicho kinasababisha pia benki hiyo kupata hasara ya mikopo waliyoitoa kwa wakulima hao.

Dk. Kimei alisema hayo jijini Dar es Salaam leo akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa mipango ya benki hiyo kwa kipindi cha mwaka jana.

“Benki ya CRDB, ni ya kwanza katika ukanda wa nchi za Kusini mwa jangwa na Sahara, kwa kuwa na mitaji 850,000 na kuwa na wateja Bilioni 1.1 na kuweza kuwakopesha wakulima wa mazao mbalimbali”alisema.

Alisema hatua ya serikali kuingilia soko la mazao ya walima pamoja na kuwalazimisha kudhalisha kwa ajili ya chakula kinawadumaza wakulima badala ya kuwajenga.

Mkurugenzi huyo. alisema ni bora wakulima wenyewe wakapewa uhuru wa kudhalisha na kuuza mazao yao katika nchi yoyote ili waweze kujiongea kipato na kuweza kulipa mikopo ya kilimo.

Alisema licha ya kuwakopesha wakulima mikopo kwa ajili ya kuboresha kilimo chao, wakulima wengi wanashindwa kurudisha mikopo hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kutokuwa na uhakika wa soko la uhakika kutokana na serikali kuingilia kati na kuwapangia bei.

Hivyo, hatua hiyo inawaumiza wakulima kwa kiasi kikubwa na kutaka serikali isiingilie kati na iruhusu soko huria kwa wakulima.

Akizungumzia juu ya utekelezaji wa mipango ya benki, alisema kwa sasa imeongeza matawi matano maeneo ya Mpanda, Ubungo, Bariadi, Mwanjelwa na Bagamoyo.

Aliongeza kwamba kwa kipindi cha mwaka jana benki imeweza kutoa mikopo ya sh milioni 700.Alisema kwa sasa wamezindia huduma ya Simbanking, ambayo mteja anaweza kupata huduma za kibenki kwa kutumia simu ya mkononi.

Alisema Simbanking inamuwezesha mteja kulipia huduma mbalimbali ikiwemo, Dawasco, Luku, na huduma nyingine.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa