Mjumbe wa CAF, Said Hamad El Maamry, ambaye alitunukiwa cheo cha heshima cha Rais wa Maisha wa Shirikisho hilo, akipongezwa na Rais wa Shirikisho hilo, Leodger Tenga. |
Makamu wa Pili wa TFF, Athuman Nyamlani, akipeana mkono na Rais wa Heshima wa TFF, Said El Maamry baada ya kutunukiwa cheo hicho cha Rais wa heshima na mkutano huo.
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Alhaj Muhidin Ndolanga, akizungumza kwenye mkutano huo baada ya kutunukiwa cheo cha heshima cha Urais wa Maisha wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwenye mkutano huo.
Alhaj Muhidin Ndolanga, akizungumza katika kuwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa kupa heshima hiyo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Leodger Tenga, akimpongeza Alhaj Muhidin Ndolanga baada ya kutunukiwa heshima hiyo na wajumbe wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment