Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Dk Aloyce Nzuki wa tatu kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na watanzania hao wakiwa wameshika vyeti vyao kushoto ni Wilfred Moshi, Respicius Baitwa wa pili kutoka kulia na Juma K. Nugaz aka Antonio Nugaz wa tatu kutoka kushoto wengine ni Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa pili kutoka kushoto.
Bodi ya Utalii Tanzania TTB leo imetoa vyeti kwa watanzania watatu walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Dk Aloyce Nzuki Akizungumza na waandishi wa habari kwa ajili ya tukio muhimu la kuwatunikia vyeti watanzania wa tatu amesema watanzania hao waliweza kupeperusha bendera ya Tanzania vizuri hasa katika masuala ya utalii, kwa hapa Tanzania na nchi za nje.
Watanzania hawa wameweza kufanya mambo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa sana yamechangia kwenye sekta ya utalii.Watanzania ambao tunaowapa tuzo leo ni pamoja na
- Mr. Respicias H. Baitwa
- Mr. Wilfred Moshi
- Mr. Juma K. Nugaz
1. Mr. Respicius BaitwaNi mtanzania wa kwanza ambaye ameweka rekodi ya Afrika kwa mwafrika wa kwanza anatarajia kupanda vilele saba virefu katika mabara yalioko duniani. Mr. Baitwa mpaka sasa ameshapanda vilele 4. Ameshapanda kilele cha kwanza Mt. Kilimanjaro zaidi ya mara 100, amepanda Elbrus kilele kirefu katika nchi za ulaya, Aconcagua, Argentina na Kosciusko Australia.
- 2. Mr. Wilfred Moshi
Wilfred Moshi amekuwa mtanzania wa kwanza kupanda kilele kirefu kuliko vyote duniani kilele cha mlima Everest. Wilifred Mosha alipanda mlima Everest mwezi may 2012 na amekua mwafrika wa 3 kupanda na kufika kilele cha mlima Everest, na kupandisha bendera ya Tanzania kwa kufanya hivyo Wilifred Mosha ameweza kutangaza jina la Tanzania na kwenye mahojiano mbalimbali na vyombo vya habari duniani ameweza kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa ujumla wake.
3. Mr. Juma K. Nugaz (Antonio Nugaz)
Juma Nugaz mtayarishaji wa kipindi cha utalii cha Kambi Popote kinachorushwa na clouds TV amekuwa mtangazaji bora katika kuhakikisha utalii wa ndani kwa mwaka 2012 tuzo iliytolewa na chama cha waandishi wa habari Tanzania.
Mr. Juma Nugaz amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kipindi cha kambi popote na amekuwa akitembelea bila kuchoka vivutio vya utalii na mwaka jana mwezi wa Disemba aliweza kurekodi kipindi maalum wakati wa zoezi la kupanda mlima kwa baadhi ya watanzania katika sherehe za kuazimisha miaka hamsimi (50) wa Tanzania bara ya Uhuru.Tunampongeza sana.
Bodi ya utalii Tanzania inawapongeza watanzania hawa kwa kufanya juhudi kubwa ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii wa Tanzania na tutaendea kushirikiana nao kutangaza vivutio vyetu zaidi.
Pamoja na kuwazawadia cheti hiki vilevile tunawazawadia safari ya kitalii kwenda mbuga za wanyama za Selous kwa siku nne na familia zao.
Chanzo: Father kidevu
No comments:
Post a Comment