Na Maneno Selanyika, Dar es Salaam
MKAZI wa Kimara Golani Jijini Dar es Salaam, Kelvin Johnson (21), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, kwa kosa la kulawiti mtoto mwenye umri wa miaka 6.
Akisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi Lilian Rugemalila, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Masini Mussa, alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 25, mwaka huu.
Mussa alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo kisha kumsababishia maumivu makali mtoto huyo katika mwili wake, huku akijua ni kosa kisheria kufanya hivyo.
Mtuhumiwa huyo alikana kosa na upelelezi wa polisi bado unaendelea, ambapo mtuhumiwa alitakiwa aje na wadhamini wawili wa kuaminika.
Mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na kuamuriwa kurudi rumande hadi Septemba 24, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
Wakati huo huo, mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, Abdul Hamidu (18), jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa miaka 18.
Akisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Flora Mtarania, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Mkude Mshanga alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Septemba 4, mwaka huu.
Mshanga alidai kuwa mtuhumiwa alifanya kosa hilo katika maficho ya Manzese, jijini Dar es Salaam, huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa alikana kosa hilo na kurudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Septemba 29, kutokana na kosa hilo kutoruhusu dhamana.

Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment