Friday, September 14, 2012

Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM)Wamaliza kikao cha baraza; Yainyooshea kidole CHADEMA kwa matukio ya mauaji



Ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
 Mjumbe
wa Kamati ya utekelezaji Taifa UVCCM,ambae pia ni mjumbe kikao Cha
Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Ridhwan
J. Kikwete akichangia hoja katika kikao Cha Baraza hilo kilichofanyika
jana, tarehe 12, Makao Makuu ya Chama,Dodoma
 Kutoka
kulia Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Ndugu Martine Shigela
akichangia ajenda katika kikao cha Baraza la Umoja huo,(katikati) ni
Makamu Mwenyekiti Ndugu Beno Malisa na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Mfaume
kizigo, wakiwa katika kikao cha Baraza hilo kililofanyika Jana tarehe
12 katika ukumbi wa sekretarieti maarufu kama (white house) uliopo
Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
 Mjumbe wa UVCCM ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani na Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdalah Ulega
 Mmoja
wa wajumbe wa Baraza ambae pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa
wa Dar es salaam, Ndugu Said Mtimizi akiwa katika Kikao hicho cha
Baraza kilichofanyika jana, Sept 12, Makao Makuu ya Chama, Dodoma.
Wajumbe
wa Baraza la UmojawaVijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wakifuatilia
hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wa kupitisha
majina ya wagombea wanafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa
na Taifa.

Baadhi ya maafisa na watendaji waUmoja waVijana,Wa kwanza kushotoNdugu
Shara Ahmed (Mkuu wa Kitengo Cha Oganaizesheni Unguja) Ndugu John Milele
(Mkuuwa Kitengo cha Fedha na Uchumi) Ndugu Deogratius Daffi (Mhasibu
Mkuu) na Ndugu Salmin Dauda(mwenye laptop) Mkuu wa Kitengo Cha
BenkiyaVijana)

Wajumbe
wa Baraza la Vijana Kutoka Tanzania, Zanzibar ambao pia ni wajumbe wa
halmashauri kuu ya Chama Taifa (NEC) wakiwakilisha vijana kutoka
Zanzibar, Ndugu Hawa Sukwa na Ndugu Hadillah Vuai (mwenye Chupa ya
maji).


Wajumbe
wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wakifuatilia
hoja kutoka kwa mmoja miongoni mwa wajumbe katika mjadala wakupitisha
majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya Umoja huo ngazi ya Mkoa
na Taifa.
Baadhi
ya wajumbe wa Kikao cha Barza la UVCCM, kutoka kulia, safu ya mbele
Salmin Dauda (Mkuu wa kitengo cha Benki ya Vijana), Tumaini Mwakasege
(Katibu Msaidizi Siasa na Oganaizesheni, Vyuo Vikuu) na Abdallah (Mkuu
wa Utawala Ofisi ndogo UVCCM, Zanzibar)
---
Na Suleyman Mwenda,

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), wamemaliza kikao cha
baraza la umoja huo ambapo wamejadili ajenda mbalimbali za msingi
kuhusu Uchaguzi na pia wamejadili juu ya hali ya siasa nchini na
mfululizo wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji, ambapo
wamekinyooshea kidole Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
kwa  kuwa vinara wa matukio ya mauaji, kitu ambacho ni hatari kwa
Taifa.



Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela wakati wa
mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi ya Katibu
Mkuu, jengo la Mikutano (whitehouse) katika Makao Makuu ya Chama Cha
Mapinduzi, Dodoma.

Alisema kuwa, kumekuwa na matukio ya mauaji kwenye mikutano ya chama
hicho katika mikoa ya Singida, Igunga, Tabora, Morogoro na Iringa hali
ambayo imekuwa ikitishia Usalama na Amani ya Nchi.



“Tunalaani Chadema kuwa vinara wa vurugu  zinazosababisha mauaji na
kila  tukio  linapotokea  viongozi  wa Chadema wanakuwepo, hali
inayoonyesha kuwa siasa wanazoendesha si za kistaarabu” alisema.



Alisema kuwa  Chadema wanachojenga ni hatari kwa Taifa  na pia hatari
kwa Umoja wa Vijana pia na kama wana mapenzi ya kweli na watanzania
waache siasa zinazasababisha mauaji mara kwa mara.



Katika hatua nyingine, Shigela amesema kuwa,Kikao cha baraza Kuu
kilimalizika jana na kufanya maamuzi baada ya kujadili na kupitisha
majina ya wagombea  na baadhi ya nafasi majina yatapelekwa halmashauri
kuu ya taifa (NEC) ambacho ni chombo cha mwisho cha maamuzi katika
Chama.



Amezitaja nafasi ambazo tayari zimetolewa maamuzi, kuwa ni nafasi ya
mwakilishi mmoja kutoka UVCCM kwenda UWT, Mwakilishi mmoja kutoka UVCCM
kwenda wazazi, Baraza Kuu taifa nafasi tano Zanzibar na nafasi tano
Bara, na sasa orodha hiyo inaandaliwa ili majina ya waliochaguliwa
yatangazwe rasmi.



Amesema kuwa,katika nafasi nyingine ikiwemo Mwenyekiti na Makamu
Mwenyekiti tayari yamewekewa alama na yatapelekwa Halmashauri kuu ya
Taifa (NEC).



Pia amewataka wagombea ambao tayari wamefanyiwa uteuzi waache siasa za kuchafuana na zile za makundi.



Aidha alisema kuwa Mkutano Mkuu wa taifa unatarajiwa kufanyika kuanzia
Oktoba 20, mwaka huu na kutaka wajumbe wote kuhakikisha wanafika Dodoma
Oktoba 19.



Shigela amesema kuwa, Baraza kuu lilipata nafasi ya kuwapongeza vijana
wa Jumuiya kwa kuthibitisha kuwa umoja huo ni tanuru la kuoka viongozi
kwa baadhi yao kuteuliwa nafasi mbalimbali serikalini na kwenye Chama
na kulitaka Baraza kuu kuzingatia mahitaji ya vijana ili wapate fursa
zaidi za kugombea ili umoja huo uweze kupeleka sura nyingi za vijana
ndani ya chama.



Pia alisema kuwa wametapa nafasi ya kuitafakari taarifa ya kazi nzuri
ya Serikali kwa kuwawezesha vijana katika suala la kuwapatia elimu na
kuwawekea mikakati ya miaka mitano ya kusaidia vijana.



Shigela aliitaka Serikali kuwa na mipango ya kudumu ili kuweza
kudhibiti majanga mbalimbali yanayotokea hapa nchini k.v mafuriko,
kuzama kwa meli, mauaji n.k.

No comments:

Post a Comment