Sunday, September 23, 2012

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI KISIMA CHA MAJI PAMOJA NA VIFAA VYA MICHEZO KWA WAKAZI WA KATA YA GONGO LA MBOTO.



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye  pia ni diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akizindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa  kwa ushirikiano wake na mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilimo Bw. Moshi Mwaluko.
Jerry Silaa akichota maji kwenye  kisima alichokikabidhi kwa wakazi wa mtaa wa Kilimo, kata ya Gongo la Mboto kama  ishara ya kufunguliwa rasmi huku baadhi ya viongozi na wakazi wa mtaa huo wakishuhudia tukio hilo.
Diwani wa kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa akimtwisha ndoo ya maji aliyochota katika kisima alichokabidhi kwa wakazi wa kata yake Bi. Hadija ambae ni mkazi wa mtaa wa Kilimo.
Jerry Silaa akimkabidhi seti ya vifaa  vya michezo kwa mmoja wa manahodha wa timu zilizoshiriki ligi ya mpira wa miguu  katika kata ya Gongo la Mboto ijulikanayo kama Jerry Super 8 na hii ni kuhamasisha michezo katika kata yake.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Gongo la  Mboto wakimsikiliza kwa makini Diwani wa kata yao Jerry Silaa (hayupo pichani) wakati akiwakabidhi vifaa vya michezo pamoja na kisima cha maji.

No comments:

Post a Comment