Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ,IGP, Said Mwema na Kamishna Jenerali wa Polisi nchini Rwanda, Emmanuel. K. Gasana.wakibadilishana Mikataba baada ya kutiliana saini ya ushirikiano wa Ulinzi baina ya Nchi hizi mbili kupiga vita uhalifu wa Kimataifa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ,IGP, Said Mwema na Kamishna Jenerali wa Polisi nchini Rwanda, Emmanuel. K. Gasana.wakitiliana saini makubaliano ya Ulinzi wa kupambana na Uhalifu wa Kimataifa kati ha Nchi hizo kupashana habari za kiulinzi, sherehe hizo zimefanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Mazizini hivi karibu.
----
TANZANIA imetiliana saini na serikali ya Rwanda juu ya mkataba wa hiari utakaoziwezesha nchi hizo kuwa na uwezo wa kuyaangalia maeneo yenye faida katika kuimarisha usalama katika mataifa hayo.
Utiaji saini huo ulifanyika katika ukumbi wa Zanziabar Beach Resort, kati ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania ,IGP, Said Mwema na Kamishna Jenerali wa Polisi nchini Rwanda, Emmanuel. K. Gasana.
Kabla ya utiaji saini huo Kamishna Msaidizi, Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, na Mkuu wa Intelijensia Makao Makuu ya Polisi, Nassor Hussein Laisser, akitoa maelezo yake alisema mkataba huo utaiwezesha Tanzania kufaidika na uandaaji wa operesheni za za kiusalama na ulinzi za pamoja.
Alisema eneo jengine ambalo litawezesha mkataba huo ni pamoja na kupeana mafunzo na ujuzi katika nyanja hizo ikiwa ni hatua zinazowesha nchi hizo kupunguza matukio ya uhalifu.
Nae Kamishna Jenerali wa Polisi nchini Rwanda, Emmanuel. K. Gasana akitoa amaelezo yake alisema nchi ya Rwanda hivi asasa imekuwa ikikabiliwa na matukio mbali mbali ya uhalifu yakiwemo wizi wa magari jambo ambalo linahitaji kupata ushirikiano.
Alisema mkataba huo utaiwezesha taifa hilo kupunguza matukio hayo huku wakijua mbinu na mafunzo yanayohitaji kwenda na wakati kwa nchi jirani.
Akizungumza waandishi wa habari IGP, Mwema alisema, Tanzania bado ina kazi kubwa kutokana na baadhi ya mataifa ya Ethopia, Sudan na Somalia kumekuwa na matukio ambayo yanaonekana kuhatarisha amani ya ukanda wa nchi hizo.
Aliseama hivi asasa kuna kesi zianazojitokeza katika matukio ya kesi za jinai ambapo watu 33 huweza kupoteza maisha jamabo ambalo linaisumbua jamii, huku wasafirishaji dawa za kulevya wakiongeza tatizo hilo na matatizo katika mipaka.

0 comments:
Post a Comment