Na Adelina Rutale na Mariamu Ayubu, Dar es Salaam.
ZAIDI ya Wajasiriamali 100 wa Mjini Dar es Salaam, wamepata mafunzo ya kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo sabuni za unga, ili kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
Akizindua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Integrated Solution and Awereness, Mahmood Omar, alisema, semina hiyo itawasaidia wajasiriamali kuondokana na umaskini na kuongeza kipato cha familia zao.
“Semina hii imeandaliwa kwa ajili ya kuwafundisha watu, ili waweze kujikwamua na tatizo hili la umaskini.
“Bidhaa hizi zitakuwa nzuri kwani hazichakachuliwi na mtu yeyote kwa hiyo Watanzania wajiandae kupokea bidhaa zetu zitakazotengezwa na wajasiriamali hawa,” alisema Omar.
Omar alizitaja bidhaa hizo kuwa ni Sabuni ya unga, maji, Shampoo, Sabuni ya kunawia mikono, karafuu, miche na zile za mwarobaini na fulana.
Naye Mele Igohe, ambaye ni mjasiriamali, alisema amefaidika na semina hizo kwani hadi sasa anaweza kutengeneza sabuni ya unga.
“Mimi nimepata faida kubwa kwani nimetengeneza sabuni na baadaye nataka ianze kuingia sokoni, bidhaa hii itanisaidia kuniingizia kipato mimi na familia yangu.
“Watu wasiogope kujiunga na semina hizi, hasa wanawake wenzangu kwani zitawasaidia kuwaingizia kipato na kutokuwategemea waume zao,” alisema Igohe.

Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment