Ukuta wa eneo la ndani ya kituo cha Mabasi ya Ubungo Bus Terminal umeangukia magari zaid ya 19 (baadhi kama uonavyo pichani) zikiwemo bajaji tatu,yaliyokuwa yamepaki eneo ambalo hutumika kupaki wakiwa wanasindikiza abiria na ndugu zao,aidha chanzo cha ajali hiyo kimeelezaa kuwa ni Mkandarasi wa eneo hilo aliyekuwa akibomoa ukuta huo,na pia imeripotiwa kuwa kuna baadhi ya majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali kwa matibabu.
Baadhi ya Maofisa kutoka Jeshi la Polisi wakiangalia baadhi ya magari yaliyoathiriwa vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta mapema leo asubuhi kwenye eneo la kupaki magari,ndani ya kituo kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani.Ukuta huo ulikuwa ukibomolewa na Mkandarasi ikiwa ni hatua za awali wa kituo hicho kuvunjwa kwa ajili ya kupisha mradi wa ujenzi wa mabasi yaendayo kasi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Afande Charles Kenyela akitoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya maofisa wa Polisi waliokuwa wamefika kwenye eneo la tukio mapema leo asubuhi
Baadhi ya watu wakiwa kwenye eneo la tukio wakishuhudia namna magari yalivyoharibika vibaya mara baada ya kuangukiwa na ukuta.
Mmoja wa watu,ambaye jina lake halikufahamika mara moja aliyeathiriwa na tukio hilo pichani kati akiwa amezungukwa na Maofisa wa jeshi la Polisi,akielezea namna hali ilivyokuwa.
0 comments:
Post a Comment