Home » » INASIKITISHA:KIJANA WA MIAKA 18 AJIUWA BAADA YA KUPATA DIVISION FOUR!

INASIKITISHA:KIJANA WA MIAKA 18 AJIUWA BAADA YA KUPATA DIVISION FOUR!

Kijana Mmoja aliye julikana kwa jina Moja tuu Barnaba aliye kuwa na Miaka 18 mkazi wa Chalambe Jijini Dar es salaam, amejiua kwa kujinyonga juzi baada ya kufeli katika mtihani wa kidato cha Nne.

Kijana huyo ambaye alitegemea kuwa angefauru kama wenzake wengine , Alichanganikiwa baada ya kuyatazama matokeo hayo yeye mwenyewe na kustaajabu kuwa amefeli.

Mwandishi wa Blogs za mikoa Akimuhoji mmoja wa rafiki zake wa karibu alisema kuwa, kijana huyo alikuwa amekwenda kumsalimia rafiki yake mmoja nyumbani kwao ambaye alikuwa na Computer ili atazame matokeo yake, aliongeza kwamba baada ya kufungua matokeo ya shule yake na kutazama alikuta wenzake wote wamefauru vizuri, nae kwa haraka haraka akachanganya namba  na kuona  kama amefauru, alitazama kwa mara tatu zaidi na alipo tazama kwa mara ya nne akagundua kuwa yeye amefeli katika mtihani huo na kuwa amepata Division Four ya point 27, na wakati huo rafiki yake aliye kuwa naye nae alikuwa amepata Division four.

Baada ya apo kijana huyo alimuaga Rafiki yake na kuondoka zake kurudi kwao, alipo fika nyumbani alimkuta mama yake na wadogo zake nyumbani, akamwambia mama yake kwamba yeye amefeli mtihani alitegemea angepata Daraja la Kwanza lakini ndio kapata Daraja la Nne na kuongeza kwamba maisha yake yatakuwa magumu sana maana mama yake hana uwezo na Baba yake amefungwa Gerezani. Mama  yake kijana huyo baada ya kusikia yote hayo alimshauri mwanae asifanye jambo lolote na kijana akaonekana kusikia.

Juzi Tarehe 19.02.2013 mida ya saa tatu asubuhi, Kijana huyo alichukua uamuzi wa kujinyonga ambapo alikwenda katika Gereji yao na kujitundika kamba Mpaka Kufa, Hata hivyo kijana huyo kabla hajafariki aliacha ujumbe unaosema kuwa'Ameamua kujiua kwa sababu ameona atakuwa hana maisha tena na hakuna mtu tena wa kuja kumtazama wala kuyajali maisha yake' 

Kijana huyu mdogo amezikwa jana Tarehe 20.02.2012

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa