Monday, March 25, 2013

MAFURIKO YAATHIRI MAKAZI YA WATU JIJINI DAR ES SALAAM





http://www.mtanzania.co.tz


 BAADHI ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam,

jana yalikumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ilionyesha jana
asubuhi. 





Mafuriko hayo yaliathiri baadhi ya makazi ya wananchi kwa kuwa maji

yalijaa katika nyumba zao.







Katika Barabara ya Mandela maeneo ya Tabata

jirani na ofisi za Gazeti la Mwananchi, maji yalijaa barabarani na kusababisha
usumbufu wa magari na waenda kwa miguu.



Kwenye maeneo hayo, magari yalikuwa yakiendeshwa kwa mwendo wa taratibu na
wakati mwingine yalikuwa yakisimama kwa vile madereva walishindwa kukabiliana
na kasi ya maji hayo.



Pamoja na hayo, hali ilionekana kuwa mbaya zaidi katika maeneo ya Ubungo
Darajani ambako maji yalikuwa yamefurika na kukaribia juu ya daraja.



Wakati maji hayo yakipita, baadhi ya mali zikiwamo magodoro, vyombo vya ndani
na samani nyingine, vilikuwa vikielea juu ya maji.



Kutokana na hali hiyo, wananchi walijaa darajani hapo wakishuhudia mafuriko
hayo na wengine wakipiga kelele kila walipokuwa wakiona mali zikielea.




No comments:

Post a Comment