Home » » MANYARA YASHINDA TAJI LA TAIFA MISS UTALII 2012/13 - VIPAJI

MANYARA YASHINDA TAJI LA TAIFA MISS UTALII 2012/13 - VIPAJI



  MREMBO Mary Rutta Pichani kutoka Mkoa wa Manyara  aliwabwaga warembo wenzake 26 katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Miss Utalii mwenye kipaji. Kinyang’anyiro hicho kilifanyika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live.


 Washiriki walio ingia tatu Bora wakiwa katika picha ya Pamoja na Mustaiki Meya wa Manispaa ya Temeke Muheshimiwa Maabad Suleiman Hoja


Jopo la Majaji wakifuatilia kwa umakini Shindano hilo




Mary Chrisostom Rutta, kutoka Mkoa wa Manyara (katikati) akifurahi baada ya kutangazwa mshindi. Kushoto ni Jamia Abdul (Kagera) na Joan John kutoka Lindi ambao waliingia tatu bora.
Mary na warembo wenzake wakishangilia ushindi huo.
Warembo wakionesha vipaji kwa kucheza ngoma za asili.
Wakionesha vazi la ubunifu.
Msanii wa ngoma za asili kutoka Bagamoyo, Chemundu Gwao, akicheza na warembo hao.
Ilikuwa ni shangwe na furaha tupu kwa washiriki na ubunifu wao.
Mwakilishi wa Kagera, Jamia Abdul, akicheza ngoma ya Kihaya.
Mikogo pia ilipewa nafasi yake mbele ya meza kuu.
Rais wa Miss Utalii Tanzania na Jaji Mkuu wa kinyang’anyiro hicho, Gideon Chipungahero ‘Chipss’ (kulia) na majaji wenzake wakikusanya pointi.
Meya wa Manispaa ya Temeke, Maabad Hoja, akimvisha Sasha mrembo huyo baada ya kutangazwa mshindi.
DJ Max (kulia) na Mc Adria Cleophace walifanya kazi kubwa ya kunogesha tukio hilo. PICHA : RICHARD BUKOS / GPL PAMOJA NA MAKTABA YA MISS UTALII TANZANIA

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa