Home » » MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI

MENEJA WA KAMPUNI YA NDEGE YA FASTJET ATIWA MBARONI




MENEJA wa
Wafanyakazi wa Ndani ya Ndege wa Kampuni ya Fastjet Emma Donovan,
alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kujibu
shtaka linalomkabili la kutoa lugha ya matusi.

Emma (40) alipandishwa kizimbani jana na kusomewa shtaka hilo na Wakili wa Serikali Nassoro Katuga, mbele ya Hakimu Joyce Minde.


Katuga alidai Machi 19 mwaka huu Emma alimtolea lugha ya matusi Samson Itinde jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Emma alikana shtaka hilo ambapo Katuga alidai upelelezi umekamilika na kuomba kupangiwa tarehe kwa usikilizwaji wa awali.
Hakimu
Joyce alisema kuwa dhamana ya mshtakiwa iko wazi lakini kwa kuzingatia
vigezo vya dhamana vitakavyotolewa kwa kuwa mshtakiwa ni raia wa kigeni.

Alitaja
masharti ya dhamana kuwa mshtakiwa anatakiwa kuwasilisha hati yake ya
kusafiria au kutoa fedha taslim sh milioni tano na pia awe na wadhamini
wawili ambao ni Watanzania.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 9 ili kupangwa tarehe ya kuanza kwa usikilizwaji wa awali.
Y

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa