Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
RAIS
Jakaya Kikwete, amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma.
Rais
Kikwete, alikabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis
Mwamunyange, Ikulu Dar es Salaam jana na ameahidi kuendelea kutafuta
vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo
cha Kijeshi kilichopo Monduli mkoani Arusha.
Maktaba hiyo ilianzishwa na Rais Kikwete, wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita.
“Lazima
mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu, lakini na mimi nitaendelea kutafuta
vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library (maktaba) yetu ya Monduli,”
alisema Rais Kikwete.
Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi,
Jenerali Mwamunyange, alimshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha
Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi.
“Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini
zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana
mafanikio haya,” alisema Jenerali Mwamunyange
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment