Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo
Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juzi baada ya
kuteuliwa kuwa msimamizi wa mkuu Wasanii wa nje ya Bunge Maalum, kulia
ni Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza nje ya bunge, Renatus Muadhi, na
katikati ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo, Agustino Matefu.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII wa Bongo Movie, muziki wa dansi, taarab, maigizo na tamthilia
wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na kamati ya Tanzania Kwanza Nje
ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza amani kwa vijana wa
rika lote bara na visiwani.
Baadhi ya wasanaii hao ni pamoja na Steven Mengele ‘Steve Nyerere’
ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa uwakilishi kwa upande wa
wasanii katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum, Muungano huo uko
chini ya Mwenyekiti Augustino Matefu.
Akizungumza juzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve
amesema kwamba ataungana na wasanii ambao wako katika vyama mbalimbali
kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR, Mageuzi , Cuf na
vyama vingine huku wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza mchakato wa
katiba uendelee huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na umoja wa
Watanzania.
Nyerere aliongeza kwa kusema kuwa yeye hakuwa na kipingamizi pindi
alipoambiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa wasimamizi wa mpango huo
ambao umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi mbalimbali za vyama
vya siasa.
“Nilipoambiwa hili jambo niliweka itikadi zangu za chama pembeni na
kuuvaa Utanzania kwanza ili kuunganisha fani zetu wote kwa pamoja na
kuweza kuwahimiza wananchi wadumishe amani tuliyokuwa nayo nchini”
alisema Nyerere.
Aliongeza pia kwa kuwaomba viongozi wa dini masheikh na maaskofu
wakiwemo mapadri wote kuungana nao wasanii hao katika kuhimizaani ya
amani ya nchi.
“Sisi wasanii tunapata riziki zetu kutokana na amani na utulivu uliopo
nchini mwetu hivyo kila msanii na Mmtanzania aone ni jambo la fedheha
kuiichezea amani ambapo siku ikipitea tutakwenda kuomba hifadhi katika
nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata ushauri kutoka kwetu”.,
Aliongeza kwa kusema kwamba ana imani kubwa watanzania watawaelewa pindi
watakapokuwa katika ziara hiyo kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na
mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa ambazo ni muziki wa taarab,
Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia. Mkutano mkubwa
unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment