Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), limekamilisha
miradi kadhaa ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikiana
na Shirika la Maendeleo la Japan (Jica).
Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin
alisema mwishoni mwa wiki kwamba miradi mikubwa zaidi ya 10
iliyofadhiliwa na JICA imeshakamilika tangu mwaka 1984 hadi sasa.
Aliitaja miradi ambayo imekamilika kuwa ni ule wa
mfumo wa usafirishaji umeme na usambazaji katika Mkoa wa Kilimanjaro
uliogharimu Sh28 bilioni.
Alisema Tanesco ilikamilisha mradi wa kuimarisha
mfumo wa usambazaji umeme kwa jiji la Dar es Salaam mwaka 1991kwa msaada
wa JICA Sh63.4 bilioni.
Severin aliitaja miradi mingine na gharama na
mwaka wa kukamilika kwake kuwa ni pamoja na wa umeme Mkoa wa Kilimanjaro
(1997 – Sh 7.8 bilioni), Mradi wa kupanua upatikanaji wa umeme kwa Mkoa
wa Dar es Salaam kwenye vituo vya kupooza umeme vya Ilala, Mbagala,
ujenzi wa Kituo cha Kariakoo na njia ya msongo wa kilovolti 132 Ubungo
hadi Ilala awamu ya kwanza (1998 – Sh 18.5 bilioni).
Mradi mwingine maarufu ni ujenzi wa kilometa saba
za msongo wa kilovolti 132 kutoka Ubungo hadi Makumbusho (2011 – Sh 7.3
bilioni), ukarabati wa kituo cha msongo wa kilovolti 132/33 cha Ilala
(2013 – Sh827 milioni), ukarabati mkubwa wa kituo cha kupooza umeme na
njia za usafirishaji umeme Mkoa wa Kilimanjaro (2013 – Sh40.6 bilioni).
Severin alitaja miradi mingine ambayo inaendelea
kuwa ni ujenzi wa mradi mkubwa wa uwekezaji kwenye usafirishaji umeme
kutoka Iringa - Dodoma – Singida – hadi Shinyanga wa kilometa 217,
kilovolti 400 maarufu kama backbone ulionza mwaka jana kwa gharama ya
Dola za Marekani 26 milioni unaotarajiwa kukamilika mwaka 2016.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment